Bukobawadau

WALEMAVU KAGERA WAHAIDIWA KUTAFUTIWA MIKOPO ILI KUPATA MITAJI YA SHUGHULI ZAO

Mkuu wa Mkoa Akiongea na Baadhi ya Wanakikundi wa BUDAP katika Ofisi yao Nyamkazi Bukoba

WALEMAVU KAGERA WAHAIDIWA KUTAFUTIWA MIKOPO ILI KUPATA MITAJI YA SHUGHULI ZAO
Katika kusistiza kauli yake kwa vitendo juu wa walemavu katika mkoa wa Kagera kujitegemea na kujishughulisha pia  kufanya kazi mbalimbali za kujipatia kipato na kuacha kuombaomba mitaani Mkuu wa Mkoa wa Kagera ametembelea kikundi cha Walemavu (BUDAP) Nyamkazi katika mji wa Bukoba ili kujionea jinsi kikundi hicho kinavyojishughulisha.
Kikundi cha BUDAP ni kikundi cha walemavu ambao wanaendesha shughuli zao za kutengeneza bidhaa mbalimbali za mikono na kujipatia kipato kwa kuuza bidhaa hizo hasa kwa wageni mbalimbali wanaofika hapa mkoani katika sekta ya utalii. Bidhaa hizo ni ngoma za asili, vidani mbalimbali pamoja na bidhaa nyinginezo mbalimbali za mikono.
Baada ya Mhe. Massawe kufika katika kituo hicho na kujionea jinsi kikundi hicho kinavyojishughulisha na kazi za mikono amehaidi kuwatafutia mtaalam wa kutengeneza andiko la mradi ili afike katika kituo hicho na kuwatengenezea andiko ambalo atalitumia kuwatafutia wafadhili ili waweze kupata mikopo kupitia andiko hilo.
Pia amewasistiza walemavu hao kubuni miradi zaidi itakayowavutia wafadhili katika kuwasaidia. Vile vile Mhe. Massawe amewahaidi kuwa ataongea na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ili naye awatembelee na kuona shughuli zao na jinsi ya kuwakwamua katika kupata mtaji wa kujishulisha zaidi.
Changamoto kubwa walionayo walemavu hao ni wenzao kuwakimbia na kutopenda kujishughulisha na kuishia mijini na kuendelea kuombaomba ambapo wanasema kuwa walianza kikundi na watu 20 lakini mpaka sasa wamebakia wanawake wawili na wanaume watano tu.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Kagera alitoa kauli ya walemavua kuacha kuwa wategezi wa kuombaomba barabarani na mijini na kutafuta miradi ya kujishulisha ili wajipatie kipato cha kujiinua wao wenyewe na familia zao waka, kauli hiyo aliitoa wiki jana Alhamisi tarehe 22/11/2012 wakati akikabidhi msaada wa baiskeli mbili kwa walemavu.
Na;         Sylvester Raphael
Afisa Habari Mkoa
KAGERA @2012
Next Post Previous Post
Bukobawadau