Bukobawadau

MAJANGA UGONJWA WA MNYAUKO WA MIGOMBA WAITESA KAGERA

 TUNAPOONGELEA mikoa ambayo imekumbana na majanga mengi hapa nchini Tanzania ambayo yameleta athari nyingi za kijamii na kiuchumi hatupaswi kuusahau mkoa wa Kagera.

Mkoa wa Kagera ambao umepakana na nchi za Rwanda, Uganda na Burundi umekuwa chimbuko la majanga mengi yanayojitokeza hapa nchini ambayo uanzia nchi jirani na hatimaye kusambaa nchini kote.

Tunaposema tunapoongelea suala la majanga hatupaswi kuusahau ugonjwa wa UKIMWI ambao kwa Tanzania ulijitokeza kwa mara ya Kwanza mkoani Kagera kabla ya kusambaa nchini kote, ulitokea nchini Uganda.

Janga la UKIMWI lilitokea nchini Uganda na hatimaye likatinga mkoani Kagera, ugonjwa wa UKIMWI ulipoingia mkoani Kagera kwa mara ya Kwanza ulikuwa ukiitwa jina la ‘Juliana’ .

Jina la juliana lilitokana na mashati yaliyokuwa yamechorwa nembo ya ndege mgogoni na kifuani yaliyokuwa yakiingizwa kwa njia ya magendo na wafanyabiashara watanzania waliokuwa wakifanya biashara na waganda maeneo ya Rukunyu

Janga jingine lililoukumba mkoa wa kagera ni lile la uvamizi uliofanywa na Rais wa zamani wa Uganda Nduli Idd Amin mwaka 1979, uvamizi huo ulileta madhara makubwa ambayo ni pamoja na vifo vya watu wengi pia ulichangia kudumaza maendeleo ya uchumi na kijamii nchini Tanzania.

Mbali na majanga yote hayo sasa kuna janga jingine jipya lililojitokeza mkoani humo ambalo limeanza kuonyesha athari nyingi ambazo ni pamoja na kiuchumi na kijamii, janga hilo sio jingine bali ni la ugonjwa wa mnyauko wa migomba unaojulikana kwa jina maarufu kwa jina la unyanjano.

Ugonjwa wa mnyauko umeanza kuhatarisha usalama wa zao la ndizi ambalo ndilo zao kuu la chakula na biashara katika mkoa humo hii inafutia hatua ya ugonjwa huo kusambaa kwa kasi ya ajabu.

Kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa unyanjano uzalishaji wa ndizi mkoani Kagera umekuwa ukipungua kila kunapokucha, migomba mingi mkoani humo imeathirika sana na ugonjwa huo ambao unaonekana kuwa tishio.

Mkoani Kagera wilaya ambazo zimeathirika zaidi kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa unyanjano ni pamoja na wilaya ya Muleba, Kyerwa, Karagwe, wilaya hizi ndizo uzalisha ndizi kwa wingi ambazo uuzwa kwenye magulio na masoko mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera, maeneo ya mikoa mingine iliyoko hapa nchini na nje ya nchi.

Mtafiti mkuu wa chuo vha utafiti wa mazao cha maruku Innocent Ndyetabula anaelezea athari zinazochangiwa na ugonjwa vwa mnyauko, anasema kufuatia kuzuka kwa ugonjwa huo hali ya upatikanaji wa ndizi kwenye masoko na magulio umekuwa mdogo sana.

Ndyetabula anasema kwa sasa kwenye magulio na masoko mbalimbali yaliyoko mkoania Kagera bei ya ununuzi wa ndizi ni wastani wa bei kati ya shilingi kati ya 13,000 hadi 30,000.

Anasema kabla ya kuzuka kwa ugonjwa wa mnyauko wa migomba bei ya ununuzi wa ndizi kwenye masoko na magulio ilikuwa na wastani wa bei kati ya shilingi 2,500 hadi 8,000 kwenye masoko na magulio na wastani wa bei kati ya shilingi 1,000 hadi 4,000 toka kwenye mashamba ya wakulima.

Anaendelea kusema kuwa upanda kwa bei ya ununuzi wa ndizi kwenye masoko na magulio umewafanya wakazi wa mkoa wa Kagera waliokuwa wanaona ndizi kama chakula chao kikuu waione ndizi sawa na mama mkwe , kwa sasa ni wahaya wachache wanaoweza kumudu bei ya sasa ya ununuzi wa ndizi.

Ndyetabula anasema ugonjwa wa mnyauko umewafanya wahaya wabadili fikira zao, kwa sasa wahaya wanaona vyakula vyote vinavyoonekana mbele yao bila kufanya uchambuzi, wahaya sasa wanakula wali, ugali na vyakula vingine ambavyo walikuwa hawavitumii hapo awali.

CREDIT;Audax

Next Post Previous Post
Bukobawadau