Bukobawadau

MTOTO ARUDISHA PENZI LA MONA, TYSON


Stori: Imelda Mtema

NDOA ya mastaa wa filamu Bongo, George Tyson na  Yvonney Chery ‘Monalisa’ iliyovunjika kitambo, ilirejewa na uhai wa saa kadhaa katika shughuli ya kumpongeza binti yao mpendwa Sonia baada ya kupata kipaimara.
Mwandishi wetu aliwashuhudia wawili hao wakionekana dhahiri kuweka tofauti zao pembeni na kujali shughuli ya binti yao iliyofanyika Jumapili iliyopita nyumbani kwa mama mzazi wa Monalisa, Suzan Lewis ‘Natasha’,  Yombo –Buza, Dar.
Muda wote walionekana wenye furaha na waliketi kwenye meza moja huku Monalisa akionesha heshima wakati wa kumlisha keki Tyson kwa kupiga magoti.
“Hawa jamani wanapendezana sana wakiwa pamoja. Jamani... mtoto wao amerudisha penzi lao. Ingefaa wakafikiria upya na kuona kuna umuhimu wa kurudiana na kumlea pamoja…
CRT;GPL
Next Post Previous Post
Bukobawadau