Bukobawadau

YALIYOJIRI: MKUTANO WA CHADEMA NA WAANDISHI WA HABARI - NOV 26, 2013

Mheshimuwa John Mnyika, Tundu Lissu na Benson Kigailla ndio wazungumzaji wakuu.

Mnyika - amewaleeza waandishi kuwa sekritarieti ya chama ilikaa kikao chake jana kujadili mambo kadhaa ndani ya chama.

Ameeleza kuwa wahusika wamesha andikiwa barua zenye tuhuma zao 11 wanazotakiwa kuzijibu ndanj ya siku 14.

Ameeleza kuwa press conference waliyofanya wamejitungia tuhuma ambazo kimsingi sizo zilizo wavua nafasi zao.

Benson Kigailla anaeleza mikakati inayoendelea kwenye kanda ambayo kimsingi ripoti zililetwa kwenye kamati kuu.

Anasema mpango na programu ya chadema ni msingi pamoja na M4C kanda unaendelea kwa mafanikio makubwa kwani misingi inaendelea kuundwa na mpaka sasa zaidi ya wakunzi elfu tisa kutoka katika kanda mbalimbali wameshafundishwa.

Wakufunzi waliokwisha fundishwa.

Taifa 30

Kanda 40

Majimbo 956

Kata 19,408

Vijiji/Mitaa 72,000

Anaeleza kuwa kuna timu nne zimeundwa kwenda kwenye kanda mbalimbali kukagua misingi iliyokwisha simikwa.

Ziwa Mashariki misingi 3069 kati 7098

Ziwa Magharibi 3840 kati 9757

Kaskazini 3278 kati ya 8417

Juu kusini 2113 kati ya 10,857

Magharibi Kata 235 kati ya kata 315

kanda ya Kati Kata 363 kati ya 495

Kanda Kusini 219 kati ya 387

Kanda ya Pwani misingi 846

Tundu Lissu.

walichokifanya kina Zitto na Kitilla ni "Diversion" mashtaka yao yanatokana na waraka wa kihaini wa mabadiliko ambao ni kinyume na katiba na maadili ya uongozi, kuvuliwa kwao nafasi zao hakuhusiani na mambo ya PAC wala kuuza nafasi zetu za wagombea kwa maccm, wala kutokushiriki kwenye ziara za chama.

anawaambia waandishi, "wamevuliwa nafasi zao na kamati kuu kwa sababu ya waraka wenye nia ovu"

Anasema chadema haijaanza kufanya maamuzi magumu leo, ilishafanya hivyo kwa Dr Walid Kaburu na kwa Chacha Wangwe na mara zote vyombo vya habari vimekuwa vinaandika kuwa CHADEMA yapasuka, mara CHADEMA inakufa lakini kipindi chote haijawahi kufa wala kupasuka, na hata kwenye hili haitakufa kama ikitokea kamati ikiwafukuza.

Lissu alieleza kuwa - Kitilla amepotosha kuwa kamati kuu haina mamlaka ya kumvua yeye nafasi yake ya ujumbe wa kamati kuu maana amechaguliwa na baraza kuu. Amesema Zitto alipaswa kumkumbusha rafiki yake maana yeye (Zitto) alikuwepo kwenye kamati kuu iliyo mvua ukatibu mkuu Dr Walid kaburu, na makamu mwenyekiti bara Chacha Wangwe. kama iliweza kwa Kaburu na Chacha Wangwe (Katibu mkuu na Makamu mwenyekiti) imeweza na kwake pia ambaye hana vyeo hivyo, hivyo aache kupotosha umma kwa makusudi.

Mwandishi mmoja aliuliza kuhusu vurugu za kuchana bendera huko Kigoma, majibu yalikuwa - kurugenzi ya ulinzi na usalama ya chama imewasiliana na viongozi wa chama Kigoma na watalitolea wao taarifa lakini taarifa za awali ni kwamba ulikuwa mpango wa kuigiza ulioandaliwa na watu waliotumwa na wameshajulikana na hatua zaidi ziko chini ya uongozi wa tawi husika.



Chadema kimewaandikia barua za kuwavua nyadhifa za uongozi Zitt na wenzie


Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kimewaandikia barua za kuwavua rasmi nyadhifa za uongozi aliyekuwa naibu katibu mkuu Mh. Zitto Kabwe na wenzie sambamba na kupewa siku kumi na nne za kujieleza kwa nini wasivuliwe uanachama kufuatia waraka wa siri walioundika na kukamatwa hivi karibuni.
Next Post Previous Post
Bukobawadau