Bukobawadau

ABIRIA WANUSURIKA KWA AJALII YA GARI WILAYANI NGARA


 Zaidi ya abiria 60 wamenusurika kupoteza maisha yao baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es salaam kueleke Bujumbura nchini Burundi kuwaka moto wilayani Ngara Mkoani Kagera.
Tukio hilo limetokea leo Desemba 18 majira ya saa tano asubuhi katika eneo la Mkajagali kijiji cha Kumuyange, nje kidogo ya mji wa Ngara na kuhusisha basi la abiria la Kampuni ya Taqwa lenye namba za usajili T 964 BHS aina ya SCANIA.

Dreva wa gari hilo Bw John Peter amesema kuwa chanzo cha moto huo  ni hitilafu katika mfumo wa breki za magurudumu ya nyuma, yaliyotoa moshi mkubwa na kuzalisha cheche zilizosababisha moto huo kutokea
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari hizi ambaye aliwahi kufika  eneo la tukio ni kwamba, mpaka majira ya saa tano na nusu asubuhi, moto huo ulikuwa umedhibitiwa na hakuna abiria aliyepata madhara
Katika jitihada za abiria na wafanyakazi wa gari hilo pamoja na watoa huduma ya kwanza kutoka idara ya afya katika Hospitali ya Nyamiaga  kuendelea kuzima moto huo baadhi ya mashuhuda wao walikazana kupora mali za abiria na kuzificha vichakani
Jeshi la polisi wilayani Ngara limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo  limefanikiwa kumtia mbaroni kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja aliyekuwa amebeba magunia madogo madogo ya bidhaa za wafanyabiashara waliokuwa wakitokea dares Salaam kuelekea mjini Ngara na Bujumbura nchini Burundi
Naye mkuu wa wilaya ya Ngara  Bw Constantine Kanyasu  naye alifanikiwa kuwasili eneo la tukio muda mfupi baada ya kutokea tukio hilo na kuwasihi madereva kuwa makini na barabara za wilaya hiyo kwa kuwa zina miteremko mikali na wapunguze mwendo kasi wakati wa safari zao
Aidha  Kanyasu amedai  kwamba  wananchi wanatakiwa kuimarisha uzalendo na kuwa na moyo wa huruma panapotokea matukio kama hayo na kuacha tabia ya udokoza kwani kufanya hivyo wanajiingiza kwenye matatizo ya kulitumikia gereza na kuathiri mfumo wa maisha ya familia zao.
Na Shaaban Ndyamukama December 18, 2013
Next Post Previous Post
Bukobawadau