Bukobawadau

ATIMIZA MIAKA 50 KATIKA UPADRE


NGARA; Waumini wa kanisa katoliki jimbo la Rulenge Ngara mkoani kagera leo wameungana na Padre Lazaro Kadende wa jimbo hilo kuadhimisha miaka 50 ya upadre katika sherehe iliyofanyika katika parokia ya Buhororo wilayani Ngara

Paroko wa parokia  ya Buhororo  Padre Barnaba Sumbuso amesema kuwa jubilee hiyo ni  kwa ajili ya kutathimini shughuli ya uchungaji wa  padre Lazaro ambaye mara baada ya kupata daraja hilo amekuwa na nyadhifa kadhaa  jimboni humo

Sumbuso amesema  kuwa waumini wanaunga  na kiongozi wao kuadhimidha miaka 50 ya upadre  ili kutafakari ufanisi wake katika  Nyanja za elimu ,Uongozi  na matumizi bora ya madarakakatika kutetea na kulinda haki za binadamu

Padre Lazaro Kadende alizaliwa mwaka 1934 kijijicha nakatunga wilayani Ngara  na kujiunga na elimu ya msingi mwaka 1944  ambapo mwaka 1945 alibatizwa kisha kujiunga na seminari mwaka 1947 huko Rubya wilayani Muleba na kuendelea 1957 huko Katigondo Bukoba
Mnamo januari 1963 alipewa daraja la ushemasi na na mhashamu askofu Joseph Kiwanuka na tarehe 18 Desemba 1963 alipata daraja la Upadre na kuanza harakati za kumtumikia Mungu na kuchunga kondoo wake kwa njia za kiroho.

Akiongea na wanahabari mara baada ya misa takatifu ya shukrani ambayo mahubiri yametolewa na padre Remijius Bukuru  padre Kadende amesema kuwa katika utumishi wake amekumbana na changamoto mbalimbali lakini amekuwa na uvumilivu katika kueneza neno la Mungu

“Niliwahi kuzama ndani ya kivuko cha mto ruvubu  pale kumwendo nikiwa bado kijana mbichi nikielekea makao makuu ya jimbo wakati ule ni jimbo la Rulenge na nilikuwa ndani ya gari lakini nilipitia mlango wa gari hilo na kuogelea nikatoka”
Amesema na kuongeza kuwa “Nawasihi vijana kuwa na uvumilivu na kulipenda kanisa katika kulitumikia”

Amesema  akiwa katika seminari ya Rubya alikuwa na wenzake 27 na alihamia seminari ya katigondo na wenzake  wanane na sasa katika  kulitumikia kanisa wamebakia mapadre wawili yeye na padre Mathias Balikwendela wa Bukoba     

Imeelezwa kuwa Padre Lazao Kadende katika utumishi wa daraja la upadre ametumikia parokia mbalimbali za jimbo la Rulenge Ngara na kuwa mkurugenzi wa elimu jimboni ,mkurugenzi wa vipindi vya radio na makamu wa baba Askofu

Hata hivyo baba askofu wa jimbo la Rulenge Ngara mhashamu Severini Niwe Mugizi ametoa rai kwa wazazi kuwapa moyo watoto wao kuwa na miito ya utume kwa kuwapatia mafunzo ya imani kupitia kwa walimu wa kiroho.
Amesema kuwa vijana pia watumie elimu na vipaji waliojaliwa na mungu bila kulazimishwa walitumikie kanisa kwani kazi ya kulitangaza neon la Mungu ni kama kazi nyingine na mafanikio yake yanajengwa na upendo kuhubiri amani na subira.
Next Post Previous Post
Bukobawadau