SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

20 December 2013

NEWS UPDATES;WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MH. KAGASHEKI ATANGAZA KUJIUZURU BUNGUNI.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi  Kagasheki amejiuzulu wadhifa wake baada ya mjadala mkali na wakina  Bungeni mjini Dodoma leo jioni.
Hii inatokana na Operesheni Tokomeza iliyolenga kuondoa ujangili uliokithiri nchini. 

Tangu kuanza kwa operesheni hiyo, kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wabunge, wanaharakati na wananchi dhidi ya askari waliokuwa wakiiendesha yakiwamo ya watu kujeruhiwa, kuchomewa nyumba, mifugo kuuawa, kupigwa na uporaji.
 
Operesheni hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa pamoja na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).
Operesheni hiyo ilizuiwa baada ya suala hilo kutinga bungeni na watunga sheria hao kuweka kando tofauti zao za kiitikadi na kuungana wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki , Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. John Nchimbi, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mathayo David Mathayo wawajibike.
Waziri Kagasheki atakumbukwa kwa kazi kubwa aliyoifanya siku za hivi karibuni katika kamata kamata ya pembe za ndovu.

1 comment:

Anonymous said...

Tunaitaji viongozi wa namna hii safi sana Kagasheki wewe ni mfano wa kuigwa

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU