Bukobawadau

TAARIFA MAALUM DEC 11,2013

NGARA
Mwenyekiti mstaafu wa chama cha mapinduzi mkoani Kagera Bw pius Ngeze amewataka viongozi wa ngazi zote kufanya shughuli za kuwaletea  maendeleo wananchi wao kwa kuzingatia uvumilivu na heshima kwa wale wanaowaongoza
 Bw Ngeze amesema hayo leo wakati akiongea na radio wanahabari mjini Ngara kuhusiana na tahimini yake ya viongozi walioko madarakani  kukiuka   misingi ya viongozi waasisi wa mataifa ya Afrika kama   JuliusK. Nyerere na  Nelson Mandela

Amesema kuwa viongozi wahakikishe wanatafuta haki na kutetea maslahi ya nchi kwa kuepuka kudhalilishana na kuvunjiana heshima mbele ya wananchi waliowapa mamlaka ya kuwatetea na kujenga utawala bora

Aidha amesema malumbano ya  kujengeana visa katika majukwa na kwenye vyombo vya kisheria kwa kuoneshana ubabe yanaweza kuwasababishia kujengeana chuki na kulipiziana visasi jambo ambalo ni hatari kiusalama


Hata hivyo Bw Ngeze amesema kuwa  viongozi wanapohitaaji ufafanuzi wa jambo kutoka serikali ama kwa wananchi  wasimame kwa kujenga hoja za msingi wakizingatia kuwa  wanayo haki kikatiba  ya kutetea maslahi ya wananchi
BIHARAMULO
Wakati wananchi wa mikoa yenye madini ya dhahabu wakichimba  madini na kupata fedha kibao yenye kukidhi mahitaji yao ya familia ,wananchi wa wilayani Biharamulo wanachimba mawe na kuyapanga barabarani ili waweze kuyauza

Mawe hayo yaliyochongwa kwa umaridadi mkubwa huuzwa ili na wao kujipatia fedha kutoka kwa madereva  wa magari makubwa watokao ndani na nje ya nchi hii  wanaokuwa wakisafirisha mizigo kutoka ama kwenda nchi za maziwa makuu.

Pamoja na kufanya hivyo bado ni waharibifu wa mazingira kwa kukata miti ovyo na kuharibu misitu hasa wafugaji wenye asili ya jamii ya kisukuma kutoka mikoa ya Geita na Shinyanga na wale wahima watokao  katika nchi  jirani ya ya Rwanda
Uchunguzi wa uliofanyika wilayani humo umebaini kuwa uharibifu wa mazingira ni wa kukata  misitu kwa madai ya kupanua mashamba ya kilimo cha mazao likiwemo zao la bangi ambalo hufichwa katika mashamba ya mahindi na mtama .

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa kagera Kanali mstaafu Fabiani Masawe ametoa agizo kwa mkuu wa wilaya ya Biharamulo Richard Mbeho kuhakikisha wafugaji na wakulima wanaokata miti ovyo kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria

Na Shaaban Ndyamukama  
December 11, 2013
Next Post Previous Post
Bukobawadau