SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

31 January 2014

AJUZA AKUTWA KAMA ALIVYO ZALIWA CHUMBANI KWA MTU!!!

Sehemu ya Wananchi wa Kata ya HAMUGEMBE  Mjini Bukoba wakiwa wamezunguka eneo la tukio  mara baada ya Polisi kufika hapo kumsaidia  Bibi Kizee baada ya kukurupushwa  chumbani kwa mtu akiwa uchi wa mnyama.
 Umati wa mashuhuda wa tukio hili
 Pichani anaonekana BI. Kizee anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70, ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, alfajiri ya leo  Ijumaa Jan 31,2014 ,Polisi wameweza kumnusuru kifo baada ya kudaiwa kukutwa akiwa uchi chumbani kwa mtu   akifanya mambo yasiyoeleweka.
Chini ya Polisi  Bibi huyo, akiwa amezingirwa na umati wa wananchi wenye hasira kali, alipotakiwa ajieleze alikotokea, alijichanganya kwa kuotoa maelezo yaliyo endelea kuzua sintofahamu
Polisi wakiondoka eneo la tukio wakiwa na  Shuhuda mmoja aliyedai alikuwa miongoni mwa waliomkurupusha bibi huyo chumbani.
 Gari la Polisi likikatiza katikati ya Mji wa Bukoba.
 Bibi mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake,mnamo alfajiri ya leo Ijumaa amekutwa akiwa  uchi wa mnyama akiwa  ndani  ya nyumba asiyo ishi wala kufahamika tena chumbani kwa mmoja wa Wapangaji wa Nyumba hiyo.
Mashuhuda wa mwanzo wanasema ,Bibi huyo amekutwa akitapatapa bila kujua la kufanya huku mwili wake ukiwa Unchi na nguo zake  zikiwa pembeni kitendo kinachopelekea kusadikiwa kwamba Bibi huyu ni  mchawi wakati wengine walidai  tusubili taarifa ya Polisi na wengine wakisema uwenda kapatwa na matamanio ya kimwili.
 Bibi Kizee huyo akiwa anasaidiwa na Polisi kushuka kwenye gari.
Kuelekea kituoni. 
 Kituo kikuu cha polisi Mjini Bukoba
Mpaka tunaingia mtamboni Bukobawadau hatukupata maelezo ya ziada ya polisi /Daktari.

3 comment:

Prudence Karugendo said...

Huyo msichana wa zamani (bibi)sio kwamba ni mchawi, hapana, ni kwamba uzalendo ulimshinda baada ya kukumbuka enzi zake akaamua aingie kwa huyo jamaa akiamini kuwa pengine angeambulia mavituz. Mnadhani mzee hana mahitaji ya kimaumbile?

Anonymous said...

Watu wenye umri huo inawezekana ni kuchanganyikiwa. Au Alzheimer...yaani ugenjwa wa akili ambao unafanya watu kusahau hata jina lao wenyewe, wake au waume zao au watoto wao. Watu wa Bukoba wenye imani za kishirikina hawawezi kuflifikiria hilo.

Panueni mawazo jamani. Uchawi hauna nguv hata kidigo.

Anonymous said...

Jamani akili nyingine.tunabidi kubadilika not everything have to be witchcraft.hivyo vitu vinatokea hata huku ulaya.huyo bibi inawezakana ni mgonjwa wa (alzheimers) but kwakuwa nyumbani hatuna hivyo vipimo kujua.alzheimers desease mtu anweza kwenda popote thinking ni kwake.wanapotewa na fahamu kwa masaa au kwa siku.ndo baadae wanarudiwa na fahamu.so what if huyo bibi its the same.

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU