Bukobawadau

JUU YA B12 NA ADAMU MCHOMVU KUTIMULIWA CLOUDS KIJANA HUYU NDIO AMESHIKA MIKOBA YAO

Raymond Mshana (25), mzaliwa wa Same,Kilimanjaro.
HIVI karibuni, watangazaji nyota waliojizolea umaarufu mkubwa Bongo kupitia Redio Clouds FM, wakitangaza kipindi cha XXL, Hamisi Mandi ‘B12’ na Adam Mchomvu ‘BabaJohn’walisimamishwa kazi kituoni hapo kwa muda usiojulikana.Inaelezwa kuwa, hata yule mtangazaji mwenye sauti yenye mvuto wa aina yake
Fatuma Hassan ‘Dj Fetty’ naye yupo kifungoni muda mrefu kabla ya akina B12 ingawa taarifa hizo hazijathibitishwa rasmi.
Katika mkumbo wa akina B12, mtangazaji mwingine wa Kipindi cha Ala za Roho,Loveness Malinzi 'Diva Loveness Love'naye amesimamishwa.Uamuzi wa kuwasimamisha B12 na Mchomvu ulifikiwa na uongozi wa Clouds kupitia Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti wa Kampuni ya Clouds Media Group,Ruge Mutahaba kwa maelezo kwamba,wamekwenda kinyume na utaratibu wa kazi ambaounaonesha vizuri kwenye mikataba yao.Pigo hilo limekuwa nafasi ya kutoka jumla kwa kijana Raymond Mshana ambaye kwa hakika anatumia nafasi hiyo vizuri sana.Raymond hutangaza Kipindi cha Top 20 kinachoruka hewani kila Jumapili kituoni hapo. Kama ni msikilizaji wa Kipindi cha XXL
kinachoruka hewani kupitia redio hiyo kila siku (kuanzia Jumatatu – Ijumaa) tangu mishale ya saa 7 mchana hadi saa 10 alasiri, utakubaliana nami kuwa jamaa anajua anachokifanya.Jambo la msingi kwa Raymond ni kufahamu kuwa uwezo anao, aongeze bidii zaidi ili aweze kupata nafasi kubwa
zaidi ya kuonyesha uwezo wake. Watu wanaweza kuona shoo zinapwaya kwa namna ama nyingine lakini si kwa ubora wa kazi – ni mazoea ya sauti za kila siku.Sishabikii akina B12, Dj Fetty na Mchomvu kuwa nje ya vipindi hivyo na ni matarajio yangu kuwa watarejea hivi karibuni lakini
iwe changamoto kwa Mshana mwenyewe,kuendelea kukaza ili azidi kuwa matawi ya
juu.Wengi hawamfahamu japo kwa ufupi.
Hapa nitakueleza japo kidogo sana ili upate kumfahamu Raymond.
 
NI NANI HASA?
Anaitwa Raymond Mshana (25), mzaliwa wa Same, Kilimanjaro. Raymond ni Mpare,moja ya makabila maarufu sana nchini.Wapare hutaniana na Wachaga ambao wote ni kutoka mkoani humo. Katika utani wao, Wachaga wamekuwa wakiwatania Wapare kuwa ni wabahili sana! Tehe..
Next Post Previous Post
Bukobawadau