Bukobawadau

BODI YA BARABARA YA MKOA WA KAGERA YAZINDUA DARAJA LA MTO KANONI MANISPAA YA BUKOBA

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Fabian Massawe akikata utepe katika uzinduzi wa  Daraja la Mto Kanoni.
 Mkuu wa mkoa wa KAGERA, Kanali mstaafu Fabian Massawe akipunga mkono mara baada ya kukata UTEPE


Kikao cha Bodi ya Barabara cha Mkoa kimefanyika mkoani Kagera na kufanya tathimini ya utekelezaji wa  ujenzi wa miradi ya barabara katika ngazi za Halmashauri na Mkoa na kujadili changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa katika kujenga, kutunza na kutumia barabara hizo.
Mkoa wa Kagera unaokadiliwa kuwa na mtandao wa barabara zenye urefu wa kilomita 7,569.24  ambapo kati ya hizo kilomita 1,914.5 zinasimamiwa na Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa na Kilomita 5,654.74 zinasimamiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Hali ya Barabara, Kwa mwaka 2013 idadi ya barabara zenye urefu wa kilomita 1,745.26 sawa na asilimia 91 zilikuwa katika hali nzuri, kilomita 166.24 sawa na asilimia 8.7 zilikuwa katika hali ya wastani na kilomita 3 sawa na asilimia 0.3 zilikuwa katika hali mbaya.
Katika Bajeti ya mwaka huu (2013/14) fedha za barabara kwa Mkoa wa Kagera jumla ya shilingi bilioni 14.89 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 9.019 zimetolewa kwa Meneja wa TANROADS Mkoa na shilingi bilioni 5.871 zimetolewa kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Kikao hicho kiliweza kujadili utekelezaji wa fedha zilizoletwa mkoani kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2012/13 pia na mwaka 2013/2014 ili kuweka mikakati ya  kuboresha utekelezaji wa miradi ya barabara.
Katika hatua nyingine wajumbe wa  kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Kagera wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera walifanya uzindizi wa daraja la mto Kanoni liloko katika Manispaa ya Bukoba.
 Katika uzinduzi huo uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe aliwasisitiza wananchi kulitunza daraja hilo bila kufanya uharibifu wa kungoa vyuma vya pembezoni na kuvifanya vyuma chakavu.
Aidha Mkuu wa Mkoa alitoa wito kwa Madiwani wa Bukoba ambao wanaendelea kugomea vikao halali vya Baraza kukubaliana na kukaa ili kupitisha maamuzi ya kuwaletea wananchi wa Maniaspaa ya Bukoba Maendeleo.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Mkoa wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Kagera Bw. Nazir Kakindo  akisoma taarifa ya ujenzi wa daraja hilo lilokamilika kwa asilimia 90 alisema likikamilika ujenzi wake utagharimu kiasi cha shilingi milioni 339,449,027 gharama hizo ni pamoja na kuweka njia ya watembea kwa miguu katika daraja la Buyekera
 Bw. Kakindo alisema Mkandarasi anayejenga daraja la Kanoni ni Mulima Construction Company ambaye anamalizia kazi ndogo ndogo zilizobakia wakati daraja hilo likiendelea kutumika baada ya kukamilika kwa asilimia 90 na kuzinduliwa leo tarehe 16/01/2014 na kuruhusiwa kuanza kutumika.
Daraja la Kanoni lilikuwa limefungwa Takribani kwa miezi mitatu kuanzia mwezi Oktoba 2013

Na Sylvestera Raphael
     Afisa Habari Kagera
 

Next Post Previous Post
Bukobawadau