Bukobawadau

BREAKING NEWSSSSS:RIPOTI YA CAG IMEMTAKA MEYA ANATORY AMANI KUJIUZURU

 Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG)yamtaka meya Anatory Amani  Kujiuzuru
 Ripoti ya CAG imemtaka meya ajiuzuru kulingana na uzito wa tuhuma nzito juu yake
Akiongea kwa niaba ya Waziri Mkuu,Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Aggrey Mwanri  amemtaka Mh Meya Kujiuzuru tu,Agrey Mwanri akiendelea kutoa maelezo ya serikali kiujumla na kukamilisha ukaguzi huo.  Watumishi wa Manispaa wachukuliwe hatua Bw. Khamis Kaputa avuliwe Madaraka Mhandisi,Mweka hazina nk wapoteze vyeo vyao! 


Mh. katika sintofahamu wakati ripoti ikiendelea kusomwa.
Mbunge Mama Mshashu kushoto na Mh. Diwani Mwajabu
Sehemu ya taswira ya kikao chenyewe ndani
Ripoti imewataka Wakandarasi wote waliopata fedha bila taratibu wazirejeshe.
 Mh. Diwani Jeanifer Badru Kichwabuta.Kikubwa alichokisema akiongea na bukobawadau ,amesema "kwake yeye haki imetendeka"
Mstahiki Meya Anatory Amani (kulia) kushoto ni Mzee Rwangisa, Ukumbuke pia Mzee huyo Luangisa ndiye aliyemwachia nafasi Meya Anatory Amani.
 Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiendelea kutoa Maelezo ya Serikali. Kuhusu Suruhisho hilo ambapo yamebainika Makosa ya Meya Anatory kufanya makubaliano bila idhini ya Madiwani na Taratibu za serikali, Basi ajipime Mwenyewe na Kujiudhuru mara moja kwa Maslahi ya Manispaa ya Bukoba.
 Baadhi ya Madiwani wakisikiliza kwa makini, kushoto ni Mh. Yusuph Ngaiza,Diwani Kashai, akifuatiwa na Mh.Mlandes kata ya Nshambya.
 Anaitwa Audax Mtiganzi ni mwanahabari aliyejitoa sana katika sakata hili
 Sehemu ya wanahabari wa vyombo mbalimbali wakiwajibika
 Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh.Fabian Massawe akitoa muda wa mapumziko baada ya Ripoti maalum kutolewa ,ikiwa ni  kukamilisha " Exit Meeting"  Cha mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali leo Januari 17.2014 Mjini Hapa, kilianza mapema saa 5 Asubuhi.
 Taswira nje ya ukumbi ilikuwa hivyi
 Sehemu ya wadau waliojitokeza kusikiliza hatima  ya kitendawili hiki.
 Hakika "Bukoba ni tanuru la Siasa"
 Mzee Kassim akifuatilia kinacho endelea.
Mwanzo wa shangwe, ndelemo na vikeleshendo nje ya ukumbi wakati wa mapumziko.
Mr  Whate pichani kulia anasema amefurahishwa sana na mahamuzi haya ingawaje yeye ni CUF.
Mdau msomaji toka jana tunakufikishia mchakato huu hatua kwa hatua ,hivyo tunachukua fursa hii kwa kutuchagua sisi kama mtandao wako wenye tija kwa habari sahihi na kwa haraka,
 Diwani Yusuph Ngaiza CCM Kashai akifurahia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG)
 Fanya fujo uone nao walikuwepo kuakikisha usalama.
 Mzee Abdul Sued( Kananga) Kagasheki akilonga  na simu juu ya taarifa ilivyo na ilipofikia
 Mh. Luangisa akielekea Mapumziko.


**Muhimu kupitia Video ya tamko la Serikali iliyopo juu  Habari hii**





Next Post Previous Post
Bukobawadau