Bukobawadau

KIKAO CHA KAMATI KUU CHADEMA KUJADILI AGENDA ZOTE JAN 3,2014.

Mmoja wa wanachama watatu wa CHADEMA waliovuliwa nafasi zao za uongozi ndani ya chama, Zitto Kabwe kupitia kwa Wakili wake, Alberto Msando, leo ameanza kufanya ‘FORUM SHOPPING’ kwa kupeleka maombi Mahakama Kuu ya Tanzania, akiomba Kamati Kuu isijadili na kuamua jambo lolote kuhusu uanachama wake, kwenye kikao maalum kinachofanyika kesho.

Awali muombaji kwa namna ambayo inaweza kuitwa kuwa ni kuvizia, alitaka Mahakama Kuu hiyo itoe amri kutokana na ombi lake hilo, bila upande wa chama kuwepo mahakamani, lakini kwa bahati nzuri mawakili wa chama, Mwanasheria Mkuu wa chama, Tundu Lissu na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala; wakafanikiwa kuwepo kortini, hivyo wakawa-served maombi hayo kisha mahakama ikalazimika kusikiliza Preliminary Objections (PO) kutoka kwa mawakili wa CHADEMA dhidi ya waleta maombi.

Maombi hayo ya wakili Msando kwa niaba ya Zitto yamefunguliwa mahakamani dhidi ya Baraza la Wadhamini CHADEMA na Katibu Mkuu wa Chama.

Hoja za mawakili wa CHADEMA katika PO zilikuwa ni katika maeneo matatu ambayo ni vifungu vya kisheria ambavyo waombaji walikosea;

1. Vifungu vya sheria walivyotumia waombaji kuomba court injunction, haviipatii Mahakama Kuu mamlaka ya kufanya maamuzi hayo wanayoomba ifanye. Kwa sababu kwa ujumla ukikosea vifungu hasa vinavyohusu msingi wa kesi, ni sawa na kwamba hakuna kesi.

2. Hati ya kiapo ya waleta maombi haikuwa na facts kama inavyotakiwa badala yake ilikuwa imejaa maneno ya ubishi ubishi.

3. Mahakama haiwezi ku-entertain kusikiliza migogoro ya ndani katika vyama vya hiari mf; vyama vya siasa, dini na michezo (ambavyo uanachama wake ni wa hiari), kwa sababu mojawapo ya principle ni kwamba ili mtu awe mwanachama anakuwa amekubaliana na katiba, kanuni, taratibu na makatazo ya chama husika.

Aidha katika maombi yake kuna vitu vingine ‘muhimu’ ambavyo mleta maombi amejikuta akivionesha kuwa anakubaliana na taratibu za chama lakini wakati huo huo tena anataka mahakama imsikilize;

· Amekiri kuwa amevuliwa nafasi za uongozi na amekata rufaa

· Amekiri kuwa ameandikiwa mashtaka kwa maandishi na yeye amejibu

· Amekiri kuwa ameandikiwa kuitwa mbele ya kikao cha Kamati Kuu ili asikilizwe utetezi wake kwa mdomo.

Kwa maneno yake hayo ni kwamba anakubaliana na na process ya chama na kwamba anajua atasikilizwa lakini tena wakati huo huo anataka mahakama imsikilize. Huo ndiyo msingi wa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA kusema kuwa kuhangaika huko ni sawa na kufanya ‘FORUM SHOPPING’.

Mleta maombi angeweza kuwa na hoja katika maombi yake iwapo angeona kuna breach of natural justice kwenye suala lake. Kitu ambacho hakijatokea na hata yeye kwenye maelezo yake anakiri hivyo.

Uamuzi wa Mahakama Kuu

Katika uamuzi wake, Jaji Utamwa amesema chama kitaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Hivyo kikao maalum cha Kamati Kuu kilichopangwa kufanyika kesho Januari 3, 2014, kitafanyika na kitajadili agenda zote (kama zilivyotolewa awali) na masuala yote yanayohusu uendeshaji wa chama, isipokuwa hakitajadili na kuamua kuhusu uanachama wa Zitto pekee, hadi Mahakama Kuu itakaposikiliza ombi lake kesho saa 3 asubuhi.

JF.
Next Post Previous Post
Bukobawadau