Bukobawadau

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AKAGUA MIRADI YA VITUO VYA PAMOJA VYA USHURU NA FORODHA NA KUTATUA KERO ZA WAFANYABIASHARA MKOANI KAGERA

Naibu Waziri Malima AKiwa Maelezo na Wahandisi wa Daiho Kuhusu Mradi
 Meneja wa Wakala wa Barabara TANIROADS Mhandisi Kalupale Akisoma Taarifa ya Mradi Mpakani Rusumo Wilayani Ngara.
 Mhandisi wa Kijapani wa Kampuni ya DAIHO CONSTRUCTION Akitoa Maelezo ya Mradi Mbele ya Naibu Waziri wa Fedha Adam Kigoma Malima
 Mitambo Ikiendelea Katika Sehemu Kitakapojengwa Kitua cha Pamoja cha Ushuru na Forodha Rusumo
Daraja la Kimataifa linalojengwa Katika Maporomoko ya Rusumo Tazama Mwenyewe

Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha  Adam Kigoma Malima alifanya ziara ya siku mbili mkoani Kagera na kukagua miradi ya ujenzi wa vituo vya umoja wa  ushuru na forodha (One Stop Border Post)Rusumo na Mtukula  na ujenzi  wa daraja la Kimataifa la Rusumo kati ya Tanzania na Rwanda.
Naibu Waziri Adam Malima  alifanya ziara hiyo mkoani Kagera kuanzia tarehe 29 -30 Januari, 2014 na kutembelea mpaka wa Rusumo Wilayani Ngara na Mtukula Wilayani Missenyi pia kuongea na wananchi na wafanyabiashara na kutatua kero zao.
Katika mradi wa ujenzi  wa Kituo cha pamoja cha ushuru na forodha  Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda Naibu Waziri alikagua ujenzi unavyoendele ikiwa ni pamoja ujenzi wa daraja la kimataifa la Rusumo ambalo ni la kisasa.
Daraja hilo llitakalokuwa na urefu wa kilometa 2 na upana wa meta 10.5 linajengwa kwa gharama ya Yeni za Kijapani blioni 2.9 na kila nchi (Tanzania na Rwanda) zinachangia fedha za Japani  Yeni bilioni 1.4 kila nchi mpaka daraja kukamilika ujenzi wake.
Kwa upande wa Tanzania mradi wote (Kituo cha pamoja cha ushuru na forodha na daraja)  umefadhiliwa na Serikali ya Japani kwa gharama  ya fedha za Japani Yeni bilioni 1.8 na  unajengwa na Kampuni ya Kijapani iitwayo DAIHO COOPERATION abapo ujenzi wake umefikia  asilimia 68.
Baada ya kukagua na kujionea ujenzi unavyoendelea Naibu Waziri Malima aliwahakikishia wananachi na wafanyabiashara kuwa serikali itahakikisha mradi huo unatekelezwa na kukamilika kwa muda uliopangwa ambapo ulianza 2 Machi, 2012 na unatarajia kukamilika 15 Novemba, 2014
Naibu Waziri  Malima aliwahakikishia wananchi na wafanyabiashara katika mpaka huo kuwa mara baada ya ujenzi wa Kituo cha pamoja cha ushuru na forodha kumilika na daraja la kimataifa kukamilika mpaka wa Rusumo  utaanzan kufanya kazi kwa masaa 24 kutoka 16 ya sasa.
Aidha akisikiliza kero za wananachi wa Rusumo waliolalamika kuhusu huduma ya maji na umeme katika mpaka huo, Naibu Waziri Malima alisema ili kituo cha pamoja cha ushuru na forodha  kifanye kazi masaa 24 ni lazima kuwepo na umeme wa uhakika katika eneo husika  na kufikia muda wa mradi kukabidhiwa kila kitu kinachohitajika kitakuwa tayari kimetekelezwa na serikali.
Katika Wilaya ya Missenyi Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alitembelea na kukagua Kituo cha pamoja cha ushuru na forodha Mtukula kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda ambacho kimekamilika ujenzi wake kwa asilimia 100 na kuanza kutoa huduma..
Kero kubwa iliyokuwa inaleta kelele nyingi katika mpaka huo ilikuwa ni umeme ambapo Naibu Waziri Malima alihakikishiwa na Meneja wa TANESCO mkoa wa Kagera Bw. Martin Maduro kuwa kufikia  tarehe 28/02/2014 umeme utakuwa tayari unawaka katika mpaka huo na mafundi wanaendelea na kazi.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Malima aliwaagiza Mamlaka ya Mapato nchini kuwajibika kwa uwazi mfano kutoza ushuru katika bidhaa mbalimbali ili kuondoa malalamiko ya wananchi  na wafanyabiashara  ambao ndiyo wateja wao au walipa kodi.
Wafanyabiashara wa Mazao walilalamika kuhusu vibali vya kusafirisha mazao kuwa vinapatikana Wizarani Dar es Salaam tu jambo ambalo linawafanya kuongeza gharama katika mazao hayo bila sababu na kumwomba Naibu Waziri Malima kuwa  vibali hivyo vipatikane katika Wilaya zao.
Akijibu suala hilo Naibu Waziri Malima alisema kuwa wizara Fedha  ikishirikiana na Wizara ya Biashara na Viwanda, na Wizara ya Kilimo wataweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha  vibali hivyo vinapatikana kilahisi ili kupunguza gharama na usumbufu kwa wafanyabiashara mipakani kwa nchi nzima.
Naibu Waziri Malima alimalizia kwa kuwahawahakikishia wafanyakazi wa mipakani katika idara zote zinazohusika katika kituo cha pamoja cha ushuru na forodha (One Stop Border Post) kuwa serikali imeanza  kutafuta ufumbuzi wa kero ya makazi yao katika mipaka ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa masaa 24 bila kuhathili utoaji wa huduma katika mipaka hiyo.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2014
Next Post Previous Post
Bukobawadau