SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

23 January 2014

PATA KUMSIKILIZA MH.BALOZI KHAMIS KAGASHEKI KATIKA MKUTANO WA HADHARA MJINI HAPA LEO JAN 23,2014(FULL VERSION 1&2)

Bonyeza kitufe cha play kusikiliza sehemu ya 1 hotuba ya Mh.Balozi Khamis Kagasheki mjini hapa leo Jan 23,2014 SEHEMU ya 2'BALOZI ASEMA HUU NI WAKATI WAKE KUIRUDISHIA BUKOBA SIO KUICHUKULIA BUKOBA'

4 comment:

mwesiga said...

nimemsikia

Anonymous said...

Nadhani Kagasheki ana shida moja kubwa,kujiamini kupita kiasi. Ilikuwa fursa nzuri ya kuunganisha wanaBukoba kuliko kumaliza muda mrefu kumkejeli Mkuu wa Mkoa. Watu wamejeruhiwa sana katika mzozo huu, ilikuwa wakati wa kuponyesha majeraha.

Benjamin Mbezi said...

Nimemsikiliza Kagasheki kwa makini sana ila ni kwa kuwa hakutoa nafasi ya watu kumuuliza maswali. Kama ningepata kumuuliza maswali basi haya ndo ningemuuliza:

(1) Je kwanini wahusika wa ujangili hakuwataja kabla ya kulazimishwa na Bunge kujiuzulu uwaziri? au alikuwa akiongoza wizara akiwa nje ya Tanzania?

(2) Je watu wa Bukoba anataka kuwaaminisha kuwa bila kamati ya Bunge kuingilia kati suala la watu waliouawa, kuteswa, na kubakwa na hata kudhalilishwa ilikuwa haki yao? kwanini asingetumia mkutano huo kuwaomba radhi watanzania walikutwa na majanga hayo? kwani hadi leo hajafanya hivyo angali alitakiwa kuwa amefanya hivyo.

(3) Je bado anahitaji watu wa Bukoba kuona kuwa alionewa kuondolewa katika nafasi ya uwaziri au alistahili kushitakiwa kwa kile kilichotokea chini ya wizara yake?

(4) Leo hii anashindwaje kuwataja wahusika wa kuuza meno ya Tembo na vipusa nje ya nchi hadi makontena yanakamatwa huko China na Ufilipino yaliyosheheni bidhaa hizo kutoka Tanzania?

Anonymous said...

Kuna maswali machache ya kujiuliza kwa hii hotuba ya Kagasheki:

(1) Je anataka kuwaaminisha watu wa Bukoba kuwa hawajui maana ya kujiuzulu?

(2) Je kwanini hakuwataja wahusika wa ujangili angali wizara aliyokuwa akiiongoza inawafahamu wahusika?

(3) Je kwanini hadi leo hajawaomba msamaha wananchi wa Tanzania kwa kile kilichotokea chini ya wizara yake? Kitendo cha watu kuuawa, kuteswa, kubakwa na hata kudhalilishwa alikifurahia? Kama hatatambua hili bado tunaendelea kufikiri kuwa naye ni miongoni mwa wahusika katika jambo hili.

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU