SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

12 January 2014

TRUST IS NOT GIVEN OR RIGHT.TRUST IS EARNEDUsikae kilasiku kumlalamikia mpenzi wako eti “mbona huniamini?” “sikuhizi umepunguza kuniamini” “utasemaje unanipenda kama huniamini?” 
‘minaona hapa hatuaminiani!” Na maneno mengine tele kisa tu umehisi huaminiwi. Jiulize kuto kuaminiwa kumeanza lini? Nini kimesababisha? Kumbuka sio haki yako kuaminiwa, na wala kuaminiwa hakulazimishwi ila mazingira ndiyo yanamlazimisha mtu kumuamini mwingine. Kamwe usitegemee kuaminiwa wakati mazingira unayojenga ni ya kuiua imani juu yako. Kabla haujaanza kulalamika kuwa huaminiwi jenga au rekebisha mazingira ya kuaminiwa kwanza. Na kama mazingira unayoyaweka ni yakutokuaminika basi usimlaumu mtu mwingine kwa kutokukuamini, jilaumu wewe mwenyewe. Usijidanganye hata siku moja kuwa kuaminiwa hushuka tu ‘automatically’ NEVER, Kuaminiwa kunaandaliwa na kujengewa mazingira.

1 comment:

Anonymous said...

Je, haiwezekani kwamba huyo asiyemwamini mwenzake anafanya hivyo sababu ya vitendo vyake mwenyewe? Kwamba yeye ndiye cheater na anafikiri na mwenzake yuko kama yeye?

Huwezi kudhibitisha kwamba watu wote wasio na imani na wenzao wana sababu nzuri ya kufanya hivyo.

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU