Bukobawadau

BREAKING NEWS: KADI Mia mbili (200) za CHADEMA kurudishwa siku ya kuzaliwa CCM Mbeya

KAMBI YA CCM GREEN GUARD, CHIMALA, MBEYA, YAVUJISHA SIRI

Kila kilichokua kinaendelea katika kambi ya CCM Chimala tulikua na watu wetu. Kamanda Beni wa mbeya mjini alifanikiwa kuingiza watu kumi;CHADEMA Chimala iliingiza makachero watatu 3. 

Kuna kadi za CHADEMA 200 ambazo zilitoka kwa Braison Mwasimba aliyefukuzwa CHADEMA ( alikuwa katibu wa tawi CHADEMA Nzovwe, Mbeya) amekabidhi hizo kadi kwa Gunza wa CCM; huyu ni mwalimu wa Wigamba sekondari (Isanga) na alikuwepo pia katika mafunzo ya Green Guard Chimala. Kadi hizo za CHADEMA wanapanga kuwapa watu siku ya maazimisho ya kuzaliwa CCM ili wazirudishe kwa J. Kikwete. Mpango huu mahusui ni kutaka kumuonyesha Kikwete kuwa CCM inakubalika Mbeya. Hii ni miongoni mwa agenda yao CCM.

CCM wamewafukuza watu kumi na tano (15) kutoka kwenye hiyo kambi, ambao nao walikuwa ni “source” wa hii habari baada ya kupigwa chini. Kati ya walio fukuzwa ni kuwa waligundulika wanatoa siri na wengine walifanya mgomo kutokana na kuahidiwa malipo ya Tsh 10,000/= kwa siku na badala yake kuwa wanalipwa 2,000/= kwa siku. 

Mambo yaliendelea kuwa mabaya baada ya chakula kuisha kambini. Ndipo mwenyekiti wa CCM wilaya, Ndg Mathayo Mwangomo alipo amua kumpigia simu mkuu wa magereza wilayani, Rujewa, na kuomba chakula. Mkuu wa magereza ali mgombeza na kumwambia kuwa usirudie kunipigia tena simu kwani shughuri za chama na magereza haziingiliani. Baada ya chakula kuisha ikabidi waanze kutumia pesa ya posho kununua mahindi na viazi. Hapo ndipo yale malipo ya 2,000/= yakakata na kukawa na mtafaruku kambini. 

Green guard walianzisha mgomo na kusema kuwa wanafanya mazoezi magumu hawawezi kurishwa viazi na wanadai fedha zao. Grean gurad waliandamana na kwenda kituo cha polisi Chimala; walikuwa vijana kama 280. Wakaambiwa waje na viongozi. Baada ya viongozi kuja wali ongea na kuyamaliza; kesho yake wakapewa 10,000/= kila mmoja. Kiongozi aliye anzaisha maandamano akapigwa chini, wakati huo vijana sita washafukuzwa.

Makachero wetu wamefanikiwa kurekodi maongozi ya makubaliano ya pesa. Pia wamerekodi walivyo kuwa wanafanya makubariano ya hizo kadi 200 hapo kambini na Ndg Mwasimba. Wamerekodi hadi maongezi ya kijana walivyo kuwa wakimfukuza na kumnyima nauli; huyo kijana anatokea Mbeya. Record tuliyo nayo ni audio ambayo itatolewa muda muafaka utakapo fika.

Kijana mmoja msamalia mwema wa Chimala ambaye anaitwa Rodi; ni kamanda wa CHADEMA aliwaone huruma vijana walio fukuzwa na bila kupewa nauli kwani walifukuzwa usiku na hawakuwa na mahala pa kulala. Alijitolea kuwarudisha mbeya mjini kwa gari lake.

Green Guard imeondoka leo, Jumamosi, February 1, 2014 kuelekea Mbeya mjini kwaajiri ya sherehe za kuzaliwa CCM.

On other note; Mathayo Mwangomo (Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Mbarali) amekuwa akiwatishia watu kuwa yeye ni serikali na atawaweka ndani. Alikutana na mwenyekiti wa CHADEMA Chimala ambaye alimchana na kumwambia yeye ni mwenyekiti wa CCM wilaya na sio serikali.

TAKE AWAY: KUNA KADI ZA CHADEMA 200 ZITARUDISHWA SIKU YA KUZALIWA CCM MBEYA. HIZI NI KADI AMBAZO ALIYE KUWA KATIBU WA CHADEMA, NZOVYWE , MBEYA, ALIKUWA NAZO. KADI HIZO HAKUZIREJESHA BAADA YA KUFUKUZWA UONGOZI

WE REPORT, YOU DECIDE
VIA Chadema Diaspora
Next Post Previous Post
Bukobawadau