Bukobawadau

HAWA NDIYO NDEGE AINA YA NYANGENYAGE WANAOZUA KIZAAZAA KATIKA KISIWA CHA MUSILA ZIWANI VICTORIA MANISPAA YA BUKOBA MKOANI KAGERA

Jamani Katika Kisiwa Kiitwacho Musila Hali ni tete kutokana na Ndege aina ya Nyange Nyange Kukivamia kisiwa hicho na kutishia maisha ya wakazi waishio katika kisiwa hicho wapatao 536.
 Pichani Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe alipotembelea kisiwa cha Musila
Aidha ndege hao wanakunya ovyo na kusababisha harufu mbaya mavi yao kutoboa mabati, pia wameua mbuzi 12, kuku 512 wamekufa, na kusababisha watu kuhara na kuharisha mara kwa mara nawakati mwingine kujisikia kuishiwa nguvu.
Pamoja na Hayo yote Kisiwa cha Musila kinachokaliwa na wananchi 536 bado walikuwa hawana vyoo hata kimoja jambo ambalo lilimfanya Mkuu wa Mkoa kutoa wiki moja kila kaya kuchimba choo chake. 
 Agizo hilo lilitekelezwa na wananchi hao kwa kuchimba vyoo 30 katika kisiwa hicho. Mkuu wa Mkoa pia amewaagiza kuandaa vifaa vya ujenzi visivyokuwa vya viwandani ili wajengewe shule na Zahanati katika kisiwa Hicho.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Inaendelea na utafiti kuhusu kinyesi cha ndege hao kuona kama kina madhara jkwa binadamu. Sampuli za kinyesi cha wananchi wa Musira kilichukuliwa ili kuchunguzwa kama kuna madhara yatokanayo na ndege hao.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2014

 
Next Post Previous Post
Bukobawadau