Bukobawadau

KANYIGO YETU LEO MARCHI 20,2014

Haya ni majengo yaliojengwa vizuri kwa mfano wa ghorofa ila kwa Sasa Majengo haya yalichomwa moto kutokana na kile kinacho aminika kuwa ni wivu wa maendeleo
Camera yetu ndani ya Kata ya Kanyigo Wilayani Missenyi,Kata ambayo Wazazi na walezi wapo katika harakati za kuandamana kupinga mwenendo wa shule ya  sekondari Kashenye iliyoshika nafasi ya mwisho kimkoa  katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2013 na nafasi ya 3166  kitaifa kati ya shule 3256
 Kijana Ashraf akichukua kumbukumbu katika jengo  hili la ghorofa ya Udongo.
 Bango la shule ya Msingi Nyungwe Kijijini Kikukwe
Barabara kuu ya Bukabuye Kanyigo kuelekea  maeneo ya jirani
 Barabara ya Kikukwe.
Mjini Kanyingo na Camera leo mtchi 20,2014
Ndani ya Kanyigo hili ni jengo lililojengwa chini ya kiwangu na kuwa na mapungufu mengi.
Hili ni ghorofa linaloendelea kujengwa katik kitongoji cha Bukoko,kata ya Kanyigo,wilaya ya Missenyi,ambalo kwa mujibu wa mhandisi majengo wilaya ya Missenyi Bw Kilawila Mboya, limejengwa chini ya kiwango na linaweza kuporomoka wakati wowote.Licha ya kuweka alama za X kuzuia ujenzi tangu mwezi Septemba 2013,ujenzi bado unaendelea na maisha ya wapita njia na watakaopanga yako hatarini.
Camera yetu ikiendelea kuangaza majengo mbalimbali ndani ya kijiji cha Bukoko kata ya Kanyigo.
Watoto kijiji hapa kama walivyokutwa na Camera yetu.
Majengo ya shule ya Msingi Kanyingo.
Bango la Shule ya Kanyigo Muslim Seminary.
 Mazingira ya Shule ya Kanyigo Muslim Seminary yenye kuonyesha ishara nzuri ya Wanafunzi wake kufaulu.


 Makazi ya mdau.
Mzee akiwajibika masikani yake.
 Muonekano wa majengo ya chuo cha Maendeleo ya Wananchi katika Wilaya za Misenyi (Gera FDC) kilichopo katika Jimbo la Nkenge



Next Post Previous Post
Bukobawadau