Bukobawadau

MZEE JAMES RUGEMALILA ATOA MIL.200/- KATIKA MAHAFALI YA TATU YA SHULE YA SEKONDARI YA KAJUMULO GIRLS HIGH SCHOOL BUKOBA

 Prof. Anna Tibaijuka kwa furaha akitoa neno.Kwa niaba ya Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea na Mwana hisa wa “VIP Engineering and Marketing Ltd” Mzee James Rugemalira aliyependa kuwa nasi leo lakini akashindwa kutokana na majukumu mengine, tunayo furaha kuwatangazia, kuwa VIP ataanzisha mfuko maalum wa kusaidia katika kuboresha utoaji Elimu katika nchi yetu, utakaoitwa “Auleria Kobulungo Muganda Memorial Education Foundation Trust”. Mfuko huu unaanzishwa kwa heshima na kumbukumbu ya mzazi wetu mpendwa marehemu Ma Auleria Kobulungo Muganda.
Mheshimiwa mgeni rasmi, Tunayo furaha kutangaza kwamba shule yetu ya Kajumulo Girls High school ndio itakuwa shule ya kwanza kufaidika na mfuko huu, na leo, VIP kwa niaba ya “Auleria Kobulungo Muganda Memorial Education Foundation Trust” imetoa jumla ya TZS 200 million (TZS 200,000,000) kwa ajili ya kuwasadia baadhi ya watoto wasio na uwezo wa kujilipia lakini wana sifa za kujiunga na kusoma katika shule hii.
Sehemu yaWanafunzi wa Kajumulo Girls High School wanaohitimu kidato cha 6 wakati wa kusherekea mahafali ya tatu katika shule yao.
 Ni matarajio yetu kuwa mchango huu utawafikia walengwa, wale watoto wenye uwezo na nia ya kusoma, lakini wanatatizwa na karo pamoja na michango mingine ya shule.
Tutashirikiana na Uongozi wa Shule na Wataalam wengine kuweka taratibu za uwazi zitakazoongoza uteuzi wa watoto watakao faidika na msaada wetu. Ninaisihi sana kamati itakayohusika na uchambuzi wa watoto wanaofaa kwa msaada huu itende kazi yake kwa uadilifu ili wale watakaochaguliwa kuhudumiwa wawe wale wanaostahili huduma hii.
Pia, ni matarajio yetu kuwa mchango wetu utakuwa kichocheo kwa watu wengine kujitoa kwa hali na mali kusaidia shule yetu hii ili iweze kupiga hatua zaidi katika jitihada za kutoa elimu bora kwa mtoto wa kike. Siku hizi watu wengi wanaweka jitihada kubwa kuzungumzia matatizo, wakati wanaweka jitihada kidogo katika juhudi za kuyatatua. Tukishirikiana kwa dhati bila shaka tunaweza kupunguza matatizo ya watoto wetu.
Kwa wale wanafunzi watakaohudumiwa na michango kama hii, ni mategemeo yetu kuwa mchango huu utawaongezea bidii ya kusoma kwa kujiamini bila mashaka kwamba watafukuzwa shule kwa kukosa karo au mahitaji mengine ya shule. Tafadhali weka juhudi ili muweze kusoma vizuri, na mukimaliza shule tuweze kuona matunda ya upendo wetu kwenu. Hakuna tunachodai kwenu, ila mafanikio yenu katika maisha.
Baba  Askofu Kilaini nae alitoa neno 
Mkuu wa Shule ya Kajumulo Girls High School Jospina Leonidace(kushoto) na kulia ni Fr. Vitus Mrosso (Nyuma) katikati ni Mr. Adrew Kagya akiwa na Balozi wa Climax Mjini Bukoba Mdau Rahym Kabyemela 
Prof. Anna Tibaijuka akiwa na Mgeni rasmi Mheshimiwa mgeni rasmi, Bi. Edwina Lupembe, Mkurugenzi wa “Mkombozi Commercial Bank" kwa furaha wakisikiliza Risala kutoka Wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita 
 Wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita(6) wakisoma Risala
 Taswira, Wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita wakisoma Risala mbele ya Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mkombozi Commercial Bank, Mama Edwina Lupembe na viongozi mbalimbali Meza kuu.
 Risala ikikabidhiwa meza kuu
 Sehemu ya Wazazi na walezi wa Wanafunzi 
 Wanafunzi wanaohitimu kidato cha 6 wakitoa burudani yao
 Raha ya kuhitimu Shule..
 Wanafunzi wanaohitimu Shule hiyo ya Kajumulo Girls High School ya Wasichana wakicheza Ngoma yao
 Ngoma ya kileo mchanganyiko wa Mtorona  kaulule kwa ladha ya Skelewu 
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mkombozi Commercial Bank, Mama Edwina Lupembe akitoa neno.
 Mr. Andrew Kagya akitoa neno.
Kwanza kabisa ni kudhihirisha kwamba VIP inagawana ndoto (VIP shares the same Vision) na mwanzilishi wa shule hii Prof. Anna Tibaijuka, ya kumkomboa mtoto wa kike ili aweze kujitegemea yeye mwenyewe, wale anaowategemea na hatimae kukomboa Taifa zima. Ni imani yetu (Conviction) kwamba njia bora ya kumkomboa mtoto wa kike ni kumpa elimu bora.

Ni njia ya kuwapa fursa watoto ambao hawana uwezo wa kifedha lakini wana sifa zinazotakiwa kupata elimu bora. Ni wakati wa kuwaonesha watoto hawa kwamba pamoja na ubinafsi unaongezeka katika jamii, bado kuna watu wanaowajali na kuwathamini. Watu ambao wako tayari kuona hata wao wanapata fursa ya kufanikiwa katika maisha. Watoto hawa wakitambua vizuri thamani ya mchango huu, wakatambua thamani ya upendo wa Taifa kwao, na hiyo itawajengea moyo wa kuwasaidia wale ambao hawana uwezo wakiwa watu wazima.

Namna nzuri ya kufundisha upendo, ni kuonyesha upendo, na namna nzuri ya kuonyesha upendo ni kwa matendo
Ngoma kutoka Ngote Wilayani Muleba  nayo ilianza kutumbuiza
Hakika Wanyayangilo wanatisha kwa kucheza  ngoma. 
Kwa hili linaloendelea kutoka Ngote hakika jirani zetu Wahamba mkajipange 
 Toka utawala wa Ntare, wahaya wametisha kwa kucheza ngoma.
Burudani ya Ngoma kutoka wanafunzi wa Kidato cha kwanza.
 Mdau mama Seleda na Mwanae.
Uzinduzi wa Jarida la kila mwaka kwa Shule hiyo ulifuata.
 Kwa hisani ya Windhoek na Climax
 
Next Post Previous Post
Bukobawadau