Bukobawadau

Ndesamburo:Ingeitishwa kura ya maoni kabla ya Bunge la Katiba

Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, amesema kabla ya Bunge la kutengeneza Katiba, serikali ingeitisha kura ya maoni ya wananchi juu ya muundo wa Muungano.

Ndesamburo ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, alisemahaoni mwelekeo wa kupata Katiba kwa kuwa suala lenye ukakasi ambalo ni muundo wa Muungano bado halijashughulikiwa nje ya Bunge kwa wananchi
kutoa maoni ya wanachokitaka.

Alisema kwa sasa muundo wa serikali mbili uliopo unazungumzia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini cha kushangaza serikali ya Tanganyika haipo na haijulikani itaundwa lini na wananchi wake hawajaulizwa lolote.

"Kwenye Katiba hii pamoja na mambo mengine suala kubwa ni Muungano...kabla ya kuja hapa serikali ingekusanya kura ya maoni ya wananchi tujue wangapi wanataka muundo upi wa muungano, Tanganyika haipo ila tunaizungumzia," alisema Ndesamburo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro.

Alisema kwa sasa ni ngumu kupata wapiga kura theluthi mbili kutoka kila pande za Muungano huku serikali ya Tanganyika ikiwa haipo ikiingizwa katika serikali ya jumla na Zanzibar ikijitegemea kama nchi.

Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya katiba, imependekeza muundo wa serikali tatu kama suluhisho la kudumu la kero za Muungano kwa kuwa muundo wa serikalio mbili uliopo una kasoro nyingi ambazo kuzitibu kunahitaji gharama ya muda na fedha nyingi.
Next Post Previous Post
Bukobawadau