Bukobawadau

TASWIRA KATIKA PICHA RAIS JK AKIHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA MARCHI 21,2014

 Rais Jakaya Kikwete, akiwahutubia Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo katika ukumbi wa Bunge mjini Dodom, ambapo katika hotuba yake ametumia dakika 155:46, kwa kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo muundo wa Katiba mpya ikiwa ni pamoja na kufafanua kuhusu shinikizo la muundo wa Serikali tatu na mambo kadhaa ya Muungano.
 Rais Jakaya Kikwete, akiwahutubia Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba

 Wajumbe wakinyanyuka kwa pamoja na kupiga makofi kumshangilia Rais Jakaya, baada ya kukonga kwa Speech yake.
  Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria 
 Mh. Freeman Mbowe akishangilia hotuba ya Rais Kikwete.
Rais Kikwete akisisitiza Jambo.
 Rais Kikwete akiendelea kuwahutubia Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
 Sehemu ya Mabalozi waliohudhuria ufunguzi huo wa Bunge la Katiba katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo jioni.
 Mama Maria Nyerere (katikati) Mama Siti Mwinyi (kushoto) na Mama Salma Kikwete, wakiwa ukumbi  humo wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete.
 Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (kushoto) Mama Tunu Pinda na Mama Asha Seif Balozi, pia wakifuatilia hotuba hiyo kwa makini.
 Rais Jakaya Kikwete, akikagua gwaride maalum kabla ya ufunguzi rasmi wa Bunge hilo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wapiga picha wakiwa bize.
 Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta na Makamu wake, Samiah Suluhu, wakijadiliana jambo wakati wakisubiri kuwapokea viongozi.
 Waandishi na watu mbalimbali wakiwa nje ya ukumbi huo wakati wa maopokezi ya viongozi mbalimbali.
 Baadhi ya waandishi
Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Next Post Previous Post
Bukobawadau