Bukobawadau

RAIS WA TFF MH.JAMAL MALINZI KUENDELEA KUWA MWENYEKITI WA (KRFA)

Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA)Jamal Emil Malinzi akizungumza na Wajumbe waliojitokeza katika mkutano huo wa Utekelezaji wa Chama cha Mpira wa Miguu (KRFA) Mkoa wa Kagera, Ambapo pia alizungumzia swala zima la kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Mkutano uliofanyika  kwenye Ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Kagera
 Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Mstaafu Issa Njiku akizungumza na wajumbe
 Pichani kushoto ni Bw. Christopher Kiiza, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji KRFA - TFF Kagera katikati ni Mkurugenzi wa Sheria na utawala Shirikisho la soka nchini TFF Mdau Evodius Mtawala.
 Chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) kimefanya mkutano mkuu wa kawaida kwenye ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Kagera na Mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Missenye Kanal Issa Njiku. 

Awali akisoma taarifa yake mwenyekiti wa KRFA ambae pia ni Rais wa TFF Jamal Emil Malinzi aliwashukuru wajumbe wote wa mkutano mkuu kwa namna walivyoshiriki kwa namna tofauti katika kuendeleza michezo katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera,Hotuba iliyosheheni mipango kedekede ya kuinua soka kwa ujumla nchini Tanzania na Kagera ikiwemo. 

Katika mambo mengi aliyoeleza ameweza kueleza changamoto nyingi zinazoikabiri KRFA na kuwataka viongozi kuhakikisha wanawasiliana na Halimashauri za wilaya zao kutenga maeneo ya viwanja vya michezo,akiongelea uwanja wa Kaitaba amesema anayofuraha kuwajulisha wajumbe kuwa sasa uwanja huo unawekewa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA kwa asilimia mia moja, Lakini pia amehaidi kuitisha Harambee ya wadau mbalimbali jijini Dar es salam kwa ajili ya kupata pesa ya kujenga jukwaa moja katika uwanja wa Kaitaba Bukoba. 
 Pia aliweza kuelezea kuhusiana na nafasi ya Uenyekiti wa KRFA, Amesema tangu amepata nafasi ya Rais TFF amekuwa akikutana na maswali mengi ya waandishi wa habari na wadau kuhusiana na kujiudhuru nafasi hiyo, (Wakati nakuja Bukoba nilikuwa na wazo ili la kujiudhuru, Lakini kila mjumbe aliesimama hapa ameniomba nisijiudhuru mpaka wengine kutamka kuwa iwapo nitajiuzuru basi nao watajiudhuru nafasi hii, lakini kuna mjumbe kasema wapo watu wakati wa kampeni walikuwa wakisema natafuta nafasi hii ili niweze kugombea urais, kwahiyo basi naomba nitamke kuwa sitojiudhuru nitaendelea kuwa mwenyekiti wa KRFA.)
 Katibu wa KRFA Saloum Umande Chama
Mdau A. Rutayuga, Mjumbe wa kamati Tendaji ya KRFA , Mjumbe wa mkutano mkuu wa TF
Mkurugenzi wa Sheria na utawala Shirikisho la soka nchini TFF Mdau Evodius Mtawala .
 Baadhi ya wajumbe wakipitia taarifa ya Utekelezaji ya Kamati ya Utendaji ya Chama cha mpira wa Miguu KRFA Mkoa wa Kagera
 Mjumbe Ndugu Jacob Kilianga Kabaijo
Mwenyekiti wa BUFA Bw. Marick Tibabimale (kushoto) na Kulia ni Bw. Jerome Simon
Picha Na Faustine Ruta, Bukoba

Punguzo  maalum la bei katika msimu huu wa sikukuu ya Pasaka, sasa unaweza kufurahia chaneli zaidi y 70 bila dish wala chengachenga, utapata king'amuzi kwa Tsh 79,000 badala ya 109,000.wahi package yako yenye kifurushi cha Tsh 40,000 bure.
 BUKOBA fika ITEMBWE GENERAL SUPPLIES wakala mkuu wa Startimes ,wanapatikana Kashozi Road, mkabala na ofisi ya MAYAWA au piga simu namba 0787 007 666/0754 760 633.
 Habari kubwa ni kwamba usipolipia unaweza kufurahia chanel 5 muhimu  za nyumbani bure kabisa!!
 STARTIMES ENJOY ULIMWENGU WA DIGITAL WA TANZANIA

.
.
Next Post Previous Post
Bukobawadau