Bukobawadau

KIZUNGUMKUTI CHA MASHINE YA KUSAGA KIJIJINI BUGOMBE KANYIGO

Mwenyekiti wa kijiji cha Bugombe Ndg Japerson Mutabuzi akiwa na Afisa mtendaji wa kijiji hicho Ndg Marwa (pichani kulia)wakifanya mawasiliano na wahusika waliofunga mashine kijijini hapa ambayo haifanya kazi,Zoezi hili limefanya wakati mkutano wa mkutano wa ukiendelea BFC
NDIYO.Ni kizungumkuti.Kikundi kiitwacho Bugombe Farmers Club katika kijiji cha Bugombe,kata ya Kanyigo kilipewa sh milioni nane miaka miwili iliyopita kutoka mradi wa DASIP(District Agricultural Sector Investment Project) wa Halmashauri ya wilaya  ya Missenyi.
Fedha hiyo iliingizwa kwenye akaunti ya kijiji ikiwa ni asilimia themanini na kikundi kikatakiwa kuchangia asilimia ishirini ili kukamilisha mradi wa mashine ya kusaga na kukoboa.
 
Kikundi hakikuruhusiwa kugusa fedha iliyoletwa bali ni DASIP kijiji waliotembeza zabuni na kununua mashine ambayo tayari imefungwa lakini kikundi hakina nyaraka zake,wala mashine haisagi kwa maana kwamba kikundi hakijakabidhiwa rasmi. Kwa mujibu wa katibu wa BFC, Said Majaliwa ,uongozi wa kijiji ni kama unawashinikiza wasaini mkataba wa Halmashauri kwamba tayari waepokea mashine,lakini kikundi kimekataa kusaini hadi mambo muhimu yawekwe sawa.
"Hatuwezi kusaini mkataba wa Halmashauri.Wanasema mashine siyo yetu moja kwa moja lakini ikiharibika tunawajibika kuulizwa,lakini hatuambiwi tunapewa muda gani wa  garantii? ," anahoji mwanakikundi Anasi Kamala.
Wanakikundi wana wasiwasi kwamba huenda wamefungiwa mashine mbovu kwa kuwa miezi miwili tangu ifungwe haijaanza kusaga. Tatizo ni nini?
Baadhi ya wanakikundi Bugombe Farmers Club kwenye mkutano wao wakitafakari mambo
 Wanakikundi wakiendelea kujadili juu ya hatima ya mashine yao, pichani kulia anayeandika ni katibu wa BFC,Said Majaliwa
Mashine ya kusaga ambayo haijafanya kazi takribani  miezi miwili tangu ifungwe licha ya wanakikundi kukamilisha kuweka umeme
Na mwanahabari Wetu;MUTAYOBA ARBOGAST,Missenyi
Next Post Previous Post
Bukobawadau