Bukobawadau

TAFADHALI PITIA HABARI HII MSAADA WAKO WA HALI NA MALI UNAHITAJIKA KWA DADA YETU!

Ndugu Msomaji wetu Ukiguswa na Habari hii tafadhali toa chochote kwa Binti huyu pichani hakika anahitaji msaada wako.Binti huyu anajulikana kwa jina la Phidea Furgence miaka 24 alijifungua watoto 3  wa kike wenye umri wa miezi 3 kwasasa.
Phidea anomba msaada wa kuwalea watoto wake ili wapate kukua kwani anasema watoto hao hawezi kuwanyonyesha maziwa ya mama tu yakawatosha wote watatu mpaka kukua. Binti huyu ameolewa na Dionizi John mwendesha bodaboda.

Pamoja na mmewe kumjali lakini anasema kipato hakitoshi kwani anahitaji pia msaidizi wa kuwalea watoto hao na kuwapatia lishe bora ndiyo maana aliamua kutembelea ofisi mbalimbali kuomba msaada.

Aidha Phidea anaishi Mtaa wa Nyangoye Manispaa ya Bukoba na mara ya Kwanza alijifungua watoto mapacha wawili wa kiume kwa sasa wana umri wa miaka 4  kwahiyo Phidea ana watoto 5 kwa sasa.Unaombwa msaada wako wa hali na mali kama fedha na mahitaji mbalimbali kama chakula kwa wtoto hawa. KumbukA Phidea hana mgogoro wowote na mmewe pia wanashirikiana vizuri ila uwezo wa kuwamudu watoto hawa wa kike watatu kwa pamoja ni vigumu ndo maana anakuomba msaada wako.
Unaweza kuwasiliana na Binti huyu kwa njia ya simu namba yake ni 0752 922 937 kama una la kumsaidia. Kumbuka binti huyu ana kazi kubwa ya kuwalea watoto wake itakuwa si busara kutumia nambayake kwa kumsumbua au kuongea mambo ambayo hayapaswi kwani ni fundi cherehani lakini ameacha kazi yake kuwalea watoto hawa.
Mungu akubariki,  tuwahurumie watoto hawa Malaika wa Bwana!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau