SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

09 April 2014

UBELGIJI WATEKETEZA TANI 1.5 ZA MENO YA TEMBO

Picha inaonesha meno ya tembo na Mtambo wa kuteketeza meno hayo. Leo hii Serikali ya Ubelgiji imeteketeza meno ya tembo tani 1.5 iliyoyakamata yakiingingizwa Ubelgiji. Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala  ameipongeza Serikali ya Ubelgiji kwa hatua hiyo na ameziomba nchi nyingine zenye soko la meno hayo kuchukua hatua kama ilivyofanya Serikali ya Ubelgiji. Aidha, Balozi Kamala ameziomba nchi zilizoendelea kusaidiana na nchi zinazoendelea kupambana na ujangiri.

1 comment:

Anonymous said...

Ya kwetu yale yaliyo kwenye "Ivory Room" vipi? Hayawaki moto au tunalangua taratibu kwa 'ndugu' zetu Wachina?

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU