Bukobawadau

WAISLAMU MULEBA WAZUIWA KUFANYA MIHADHARA

Shekhe wa wilaya ya Muleba Zacharia Kagimbo
 MULEBA: WAUMINI wa dini ya kiislamu katika mji wa Muleba Mkoani Kagera juzi  wamezuiwa na jeshi la polisi wilayani humo kuendelea na mhadhara wa dini yao kwa madai kuwa ulilenga kukashifu dini ya Kikristu
Wakiongea naMwanahabari hizi katika mji huo nchi waumini hao walisema kuwa mhadhara huo wa siku tatu katika mji wa Muleba uliendeshwa na wahadhili kutoka jijini   Dar es Salaam  wakilenga kubainisha ukweli baina ya Uislamu na Ukristo.  

Imamu wa msikiti wa ijumaa  wa Masjidi Nuru aliyejitambulisha kwa jina la Issa bin Sued katika mji huo alisema kuwa mtafaruku huo ulichangiwa na kiongozi wa BAKWATA wilaya  ya Muleba Sheikh Zacharia Kagimbo  kutopenda mhadhara huo

Alisema katika kutoa mhadhara huo wahadhiri walifafanulia waislamu kuwa katika uislamu mwenyezi Mungu alikuwa na manabii wengi   kabla na baada ya kuwepo mtume Mohamadi saw na kwamba miongoni mwao ni nabii Issa mwana wa Mariam

Alidai mara baada ya  waislamu kuhudhuria na baadhi ya wasikilizaji wa imani ya kikristo walianza kulalamikia mhadhara huo  kwa  kusikia kuwa nabii Issa sio Mungu wala mtoto wa Mungu kama wasemavyo waumini wa dini nyingine

Aidha alisema kuhusiana na hali hiyo wakristo walilalamika hata kwa mbunge wa jimbo la Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka   na mkuu wa wilaya kisha  kumfuata shekhe wa wilaya ya Muleba Zacharia kagimbo  na kulalamikia hilo

“Wahadhili walikuwa na vibali kwani walishazunguka nchi nzima kwa mkoa wa Kagera walisha pita wilaya nyingi hivyo kuzuiliwa ni kuwakosesha haki kupata elimu ya dini yao”.Alisema Imamu Issa Sued.

Aliongeza kusema kuwa wakati mhadhara wa dini ukiendelea waliona jeshi la polisi likiwafikia wahadhiri hao na kuwataka wafunge vilago kuondoka  kwani mahubiri yao yanalenga kuhatarisha usalama wa kiimani baina ya dini mbili


Kwa upande  Hilali dini   Kipozeo ambaye ni mmoja wa wahadhiri na makamu mwenyekiti  wa Mihadhara kanda ya ziwa katika kulingania waislamu alisema hawakuwa na nia ya kukashifu dini nyingine bali wanaeneza dini yao.

Alisema kuwa jeshi la polisi lilifika kwa shinikizo la viongozi wa serikali na kiongozi wa BAKWATA wilayani Muleba na kwamba hakuna mhadhiri aliyeumizwa wala kuamatwa na malengo yao ni kueneza dini kupata waumini wengi wa kiislamu

“Mtume Mohamad SAW alipata mitihani wakati akieneza dini ambapo aling’olewa na meno  hili sio geni  kwetu kwani ulimwengu huu vita kubwa ni kuangamiza uislamu”.Alisema Kipozeo

Alisema kuwa safari ya wahadhiri hao imelenga kwa mikoa ya kanda ya ziwa ambapo kwa mkoa wa kagera walishatembelea wilaya ya Biharamulo Karagwe Muleba Bukoba manispaa Misenyi hadi Kampala nchini Uganda.

Hata hivyo Kiongzo wa BAKWATA  wilayani Shekhe Zacharia Kagimbo amekanusha kutohusika na vurugu hizo na kwamba hakuwa na taarifa za kuwepo kwa wahadhiri hao kueneza dini yao na kusambaza ujumbe wa Allah SW.

Alisema taarifa za kuwepo vurugu  za mhadhara alizipokea kutoka jeshi la polisi ngazi ya wilaya hasa kwa OCD na kwamba hakuna kiongozi wa mtaa wa Muleba mjini wala msikiti wa Nuru aliye mtaarifu kuwepo kwa wageni hao

Alishauri kwa wale wanaohitaji kueneza dini ya kiislamu wilayani humo kuzingatia taratibu kwa kuwaona viongozi wanaohusika na maeneo ikiwa ni pamoja na kupitia kwenye vyombo vya usalama ili kulinda amani na utulivu kwa dini zote.
Na shaaban Nassibu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau