Bukobawadau

MAREKANI YAIWEKEA UGANDA VIKWAZO KUHUSIANA NA SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

 Sekta ya Afya na usalama wa taifa itaathirika na vikwazo hivyo.
Marekani imeiwekea Uganda vikwazo kwa kupitisha sheria zinazopinga mapenzi ya jinsi moja katika taifa hilo la Mashariki ya Afrika.
Afisa wa mahusiano anayesimamia maswala ya usalama katika ikulu ya whitehouse Caitlin Hayden anasema kupitia kwa barua kwa wanahabari kuwa sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la Uganda mwezi Februari inakiuka haki za binadamu.
 Vikwazo hivyo vitajumuishwa marufuku ya wanaharakati waliopigia debe sheria hiyo kupitishwa kutoingia Marekani.
Miradi itakayoathirika na marufuku hiyo ni pamoja na ushirikiano na polisi wa Uganda Wizara ya Afya.
Aidha msaada kwa miradi iliyoanzishwa kwa usaidizi wa marekani pia utapunguzwa mbali na kufutiliwa mbali kwa mazoezi ya kijeshi kati ya majeshi ya uganda na yale ya Marekani.
Sheria hiyo inaharamisha uhusiano baina ya watu wa jinsia moja na wale watakaopatikana wanaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
Hii ndiyo hatua ya hivi karibuni iliyochukuliwa na Marekani katika ajenda yake ya kupinga sheria hiyo mpya nchini Uganda.
Juma lililopita Seneta mmoja kutoka Marekani ,Kirsten Gillibrand alilalmikia vikali uteuzi wa waziri wa maswala ya kigeni wa Uganda Sam Kutesa kuchaguliwa kuwa rais wa Umoja wa Mataifa kutokana na kuwa anatokea Uganda.
Marekani imeiwekea Uganda vikwanzo kuhusina na sheria ya wapenzi wa jinsia moja.
Watu 9000 walikuwa wametia sahihi pendekezo la kuitaka Umoja wa Mataifa kumng'oa kitini bw Kutesa aliyechaguliwa licha ya kampeini hiyo.
Wanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja wameenda mahakamani wakitaka sheria hiyo iondolewe lakini inatarajiwa kupingwa kwani rais Yoweri Museveni aliupitisha maksudi kudhihirishia wafuasi wake kuwa yu huru kutokana na shinikizo kutoka kwa mataifa ya ughaibuni .
Punde baada ya kupitishia kwa sheria hiyo mpya benki kuu ya dunia iliahirisha utoaji wa mkopo wa dola milioni 90 ambazo zilikuwa zinapaswa kutumika kuimarisha sekta ya Afya nchini Uganda .
Mataifa mengi tu ikiwemo Denmark, Norway, Uholanzi na Sweden zote zimekatiza msaada kwa taifa hilo la Afrika Mashariki.
Next Post Previous Post
Bukobawadau