Bukobawadau

PICHA VURUGU ZA WAMACHINGA JIJINI MWANZA

 Jeshi la Polisi Jijini Mwanza,leo June 11, 2014,asubuhi. limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara wadogo  maarufu  kama  machinga waliokuwa wakipinga kuondolewa katika eneo la Kempu na eneo la soko la Makoroboi jijini Mwanza.
 Hatua hiyo imesababisha vurugu kubwa na kusimamishwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo kufungwa kwa maduka hadi katikati ya eneo la jiji na baadhi ya huduma ya usafiri kukosekana kwa muda katika barabara zinazokatiza katikati ya jiji  kuanzia saa nne asubuhi .
 Mabomu ya machozi yarindima zaidi ya masaa 3.
 Mabomu ya machozi yatumika kuwatawanya machinga na kusimamishwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii.


Next Post Previous Post
Bukobawadau