Bukobawadau

KWA MORALI MIEMBENI YAWASHIDA KASHAI 5-4 NAKUTINGA NUSU FAINALI #KAGASHEKI CUP

 Ndani ya Uwanja wa Kaitaba  WADAU wa soka wakiwa tayari kufuatilia mchuano wa hatua ya Robo fainali KAKASHEKI CUP 2014 kati ya Kashai na Miembeni,pichani ni Ndugu Jamal Kalumuna, Ndugu Jumanne Bingwa na Ndugu Optaty Henry(Katibu)
Ndugu Moa Nyundo Kiongozi wa Timu ya Kashai iliyotembezewa kichapo na Vijana wa Miembeni.
 Blogger Mc nikiteta jambo na Kaka Mkuu Ernest Nyambo kuhusiano na mpambano wa leo
 Kikosi Kamili cha Wachezaji wa Miembeni
Kikosi Cha Kashai maarufu kama Wanyaluganda
Twende wote mpaka mwisho wa habari upate taswira kamili Uwanjani Kaitaba leo
 Benchi la Timu ya Vijana wa Miembeni walioweza kufudhu hatua ya Nusu fainali
Timu ya Miembeni imeweza kufanya kile kilichotegemewa na kukata tiketi ya kucheza nusu fainali, kwa kuwatoa BANYALUGANDA 'Kashai'kwa penati 5-4 baada ya kwenda sare ya 1-1 katika dakika 90 za mchezo wa robo fainali yenye Viwango na kusisimua iliyochezwakatika uwanja wa Kaitaba Jioni ya leo Jumapili July 27,2014
 Mwenye Kofia ni Kocha wa Kashai Mshindo Madega mchezaji Zamani RTC Kagera
 Benchi la Ufundi  Timu ya Miembeni
Benchi la Ufundi Timu ya Kashai
 Licha ya ushindi huo,Miembeni  walipoteza nafasi nyingi za kufunga na zikiwa za wazi kipindi cha kwanza ambapo mshambuliaji wake akipoteza nafasi mbili na nyingine mpira ukigonga Mwamba
Mtu na mtu, tambo kwa hatua.
 Mpaka Mapumziko Kashai 0-0 Miembeni
 Mchezaji wa Miembeni kuelekea mapumziko
Wachezaji wa Kashai Kuelekea Mapumziko.
Ni mapumziko baada ya dakika 45 za Kipindi cha kwanza.
  Mh.Yusuph Ngaiza Diwani Kashai akiteta jambo na kocha wa Kashai Mshindo Madega.
 Mwanalibineke wetu nikatumia Kipindi cha mapumziko kufanya Ukodak wa hapa na pale .
 Kila kona  na Mie  niwemo namieee jamani!!
 Mbele ya Jukwaa kuu nakutana na Mdau pichani
Kutoka Kushoto ni Sady Idd, Super Self Mkude, Kaka Mkubwa Ernest Nyambo wakiwa wametumia sawia ngoma safi au tshert zenye nembo ya Bukoba Veterans.
Ndugu Masala na Ndugu Amini Idrisa pichani5-
 Mwenye tabasamu ni Mdau Ashiru Abdallah
 Kipindi cha pili mambo yalibadilika kabisa ambapo Kashai waliingia kwa kasi na kucheza pasi zao fupi fupi na za uhakika na kupata bao mnamo dakika ya 70. 
 Nikiakikisha Sura za mashabiki wa Miembeni
Wachezaji wa Kashai wakiendelea vizuri kwa kutawala katika nafasi ya Kiungo
Mpira ukiendea kwa kasi.
Malick Sudi Tibabimale akifuatilia Soka na Sehemu ya mashabiki Jukwaa la Mchanganyiko
Jukwaa la Golani, sehemu kubwa ya mashabiki wa Bilele wakitoa Support kwa Miembeni 
 Goaal, ni Mashabiki wa Kashai kwa shagwe za aina yake wakishangilia bao lao la kwanza.
Mashabiki wakipokea kwa shangwe bao la kwanza la Kashai
 Hii ndiyo hali kwa mashabiki wa Kashai.
Hakika michuano ya Kagasheki Cup inagusa hisia za mashabiki kwa kiasi kikubwa sana!!
 Wachezaji wa Miembeni wakimlalamikia muamuzi wa pembeni.
 Bao la kwanza la Kashai , lilionekana kuwachanganya sana Wachezaji wa Miembeni
#Team BukobaWADAU tukiendelea live Uwanjani Kaitaba.
Hakika ni hali ya taflani Kwa Wachezaji wa miembeni dhidi ya Waamuzi.
Ndugu Sajidu Kashai
Sehemu ya Mashabiki Jukwaani.
 Swagar za Kijana Rama Sudy Lilai shabiki wa Kashai


 Kutoka 88.5 Kasimbante Fm Radio ni Mtangazi Abdulrazak Majid akirusha matangazo Live.
Mwana wa Kashai Thomas akiwa kajitenga na kuendelea kufuatilia mpambano, 

 Haaaahhhh ni wachezaji wa Benchi la Kashai wakilalmikia maamuzu ya Uwanjani
Kona kuelekea katika lango la Timu ya Miembeni. 
Mlinda Mlango wa Timu ya Miembeni akiokoa penati na kupelekea matokeo ya 5-4 
 Mshambuliaji wa miembeni Jezi namba (3)Mgongoni akiwa tayari kutupia penati yake wavuni.
 Gooooal Miembeni 5-4 Kashai.
 Mashabiki wakishuhudia namna nyasi zinavyotifuka ndani ya Uwanja wa Kaitaba
 Mc Jerry pichani na Mdau Buruhani Bushako (Ras Bitto)
Sehemu ya picha za mashabiki wakiwa Jukwaani
 Taswira mbalimbali Uwanjani Kai
 Mwisho ni Sehemu ya Mamia ya watu waliojitokeza Uwanjani wakitafuta njia ya kutokakea.
Timu nzima ya Bukobawadau Blog tunawatakieni Maandalizi mema ya Siku Kuu ya Idd


Next Post Previous Post
Bukobawadau