Bukobawadau

LEO AUG 13, 2014 NI KUMBUKUMBU YA MIAKA 11 YA KIFO CHA LEGENDARY JUSTIN KALIKAWE KILICHOTOKEA AUG 13, 2003

R.I.P Justini Kalikawe
Kwa siku ya Jana nikiwa katika kutoa ushirikiano kwa Wadau wa Clouds TV juu ya mambo kadha wa kadha mjini hapa wakiwa katika maandalizi ya Tamasha la fiesta,niliweza kufika nyumbani kwa mjane wa Marehemu Kalikawe Bi Georgia Kalikawe maarufu kwa jina la mwanae mkubwa yaani 'Mama Abayo' ambapo ameweza kuelezea mengi na mikakati aliyonayo juu ya kazi za Marehemu Justin Kalikawe na kuongeza kwamba leo Jumatano ni kumbukumbu ya miaka 11 tokea kifo chake.
"Nilikuja kutafuta ugenini, nikazoea pakawa ni nyumbani, sasa ninaelekea uzeeni, nibaki huku au nirudi nyumbani. Nilioa nikazaa na watoto, na nilipotoka kwao ni kama ndoto; lakini najiuliza siku nikirudi kwetu, niende nao au wabaki huku"
Hayo ni maneno anayoanza nayo mwanamuziki aliyepata kufanya vvema saana katika miondoko ya Reggae nchini Tanzania Marehemu Justine Kalikawe katika wimbo wake Kitendawili. Kama ilivyo kwa nyimbo nyingi ambazo zinakuwa na UJUMBE HALISI wa maisha kwa hadhira, wimbo huu bado unaendelea kuwa na maana na mguso uleule kwa wale walio mbali na nyumbani na hasa wale walioanzisha familia ambapo ikifika suala la maisha baada ya kustaafu unarejea kujiuliza kama alivyojiuliza Kalikawe.
Haijalishi alitunga wimbo huu akiwa wapi, ama akijifikiria kama aliye wapi, lakini kwa kuwa alifanya kile afanyacho vema zaidi kwa kutunga nyimbo zenye uhalisia kwa jamii, bado sasa hivi ndugu wengi tulio mbali na nyuni tukiusikiliza wimbo huu tunapata hisia halisi ya alichoeleza Justine na kuweza kujiuliza maswali ambayo naye aliuliza kwenye utunzi wake huu, bado ujumbe wake unawagusa wengi ambao kwa bahati mbaya kutokana na mfumo wa maisha ya sasa wameelekea popote duniani kwa namna yoyote kusaka chochote ili kuweza kurejesha uwekezaji nyumbani, na kama ilivyo kwa binadamu yoyote, unapofika mahali ndio unaapoanzisha urafiki na "udugu" na uliokutana nao, na wakati muafaka ukifika unaanzisha familia na kwa majaaliwa ya Mungu unapopata watoto inakuwa baraka, lakini baadae waweza kujiuliza kama aliyojiuliza Kalikawe kuwa
"nilikotoka niliishi na wazazi, babu na bibi, mjomba na shangazi, lakini huku mimi na familia, ndugu wengine ni eneo la kazi eeeee; katikati kuna bahari, tena ni mbali elfu kumi maili, nikisafiri nafika alfajiri tena ni mbali natumia utajiri eee"
Sijui la kusema, lakini namkumbuka Justine kama moja ya nguzo za muziki wa Reggae mkoani Kagera na Tanzania kwa ujumla. Alitumia lugha zake za Kihaya na Kiswahili kufikisha ujumbe aliokusudia kwa jamii husika na mara zote ALIELIMISHA, AKIBURUDISHA NA AMA KUIFUNZA JAMII KUJIKOMBOA KUTOKA KATIKA UTUMWA WA KIAKILI. Justine alifariki ghafla mwezi wa nane mwaka 2003 katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Kagera mjini Bukoba miezi michache baada ya kurejea kutoka ziara ya kimuziki nchini Denmark. Aliacha mjane Georgia na watoto wawili Abayo na Niwe na mpaka mauti yanamkuta alikuwa ndiye msanii mwenye albamu nyingi zaidi za Reggae nchini Tanzania (8 za audio na 3 za video katika miaka 16 aliyodumu katika muziki wa Reggae). 
Katika kumuenzi, wasanii nyota wa Reggae nchini walitunga wimbo wa HAKUNA na kuandaa Tamasha maalum la kuenzi kazi na maisha ya Justine lililofanyika Don Bosco. Tulishapata kujadili FIKRA PEVU / MAONO ya Justine Kalikawe katika wimbo wa HAKUNA kwa kuhusisha na uchaguzi ujao
Credit;Muberwa Bandio
Pichani Mjane wa Marehemu Kalikawe Bi Georgia Kalikawe akiongea na CLOUDS TV.
kutoka Clouds Media Group wakiendelea kufanya interview na Mke wa Marehemu Justin Kalikawe
Mdau kutoka Clouds Tv akiwajibika katika kaburi la Marehemu Justin Kalikawe.
Marehemu Justine Kalikawe alipotwaa tuzo ya msanii bora wa Reggae
,Hivi ndivyo mazishi ya marehemu Justine Kalikawe yalivyokua , kijijini kwake KITENDAGULO Mjini Bukoba.
Meneja uendeshaji wa kampuni ya utalii ya Kiroyera,Ndugu William Rutta akitolea jambo ufafanuzi kwa wanahabari wa Clouds Tv waliopo mjini hapa ikiwa harakati za kusambaza upendo sasa zinahamia bukoba kwa siku ya ijumaa hii ya tarehe 15 mwezi huu, na kahama ambapo itakuwa siku ya jumapili ya tarehe 17 mwezi huu. sasa nikupe mchongo wa mastaa wako utakaoweza kuwashuhudia; Ommy Dimpoz,Young Killer,Barnaba,Madee,Jux,Ney wa Mitego,
Stamina,Mr. Blue,Recho,Linah,Super Nyota, Khadija wa Maumivu ,BK sunday na Saida Karoli
Kumbuka, shangwe hili lote utaweza kulifaidi kwa kiingilio cha shilingi 5000 tu itakayokupa nafasi wewe mkazi wa Bukoba kupenya ndani ya Kaitaba Stadium na kwa wewe mkazi wa Kahama kujichanganya kahama stadium sehemu pekee ambapo historia ya fiesta ya kwanza itaandikiwa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau