Bukobawadau

BALOZI KAMALA AKUTANA NA SENETA WA KWANZA MWAFRIKA KATIKA BARAZA LA SENETI YA UBELGIJI

Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kushoto) akimkabidhi Seneta wa kwanza Mwafrika katika Baraza la Seneti la Ubelgiji Mhe. Bertin Mampaka. Seneta Mampaka vilevile ni Spika wa Bunge la Brussels na pia ni Mbunge wa Bunge la Walonia la Ubelgiji. Balozi Kamala amemuomba Seneta Mampaka kuitangaza vizuri Tanzania katika Baraza la Seneti la Ubelgiji, Bunge la Brussels na katika Bunge la Walonia. Aidha, Balozi Kamala amemuomba seneta huyo kuhimiza makampuni mbalimbali ya Ubelgiji kuwekeza Tanzania. Balozi Kamala yuko kwenye ziara ya kikazi ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Ubelgiji na kukutana pia na viongozi mbalimbali wenye ushawishi katika masuala ya Kitaifa,  Kimataifa  na Jumuiya ya Ulaya.
Next Post Previous Post
Bukobawadau