Bukobawadau

GUMZO NI MJENGO MPYA WA BALOTTELLI

 Mario Balotelli ndio kwanza amerejea England, kwa mara ya pili, lakini inaonekana haijamchukua muda mrefu kugonga vichwa vya habari, safari hii kwa kuonesha "ladha" ya mitindo na mambo anayopenda.
 Mchezaji huyo wa Liverpool aliyenunuliwa kutoka AC Milan kwa pauni milioni 16, amekuwa akitafuta nyumba, na inasemekana ameichagua hii (katika picha) iliyopo nje ya mji, - eneo la Helsby, Cheshire
 Kupitia picha hizi  pamoja na habari ambazo zimeandikwa na magazeti na tovuti kadhaa hapa Uingereza ni za kuaminika, basi inaonekana Balotelli ameonesha 'staili' yake kwa 'kuteua' jumba hili ambalo thamani yake ni pauni milioni 4.7.
 Nyumba hii ina vyumba vitano, ikiwa pamoja na kila kitu ambacho mchezaji soka , Kijana, milionea anahitaji. Vitu 'muhimu' kama bwawa la kuogelea, sauna, chumba cha kuhifadhia mvinvyo (wine cellar), sehemu ya kutua helikopta, uwanja wa mpira.. Na vingine 'vidogovidogo'.
 Mpaka hapo hatuna la kuongea ,ndivyo unavyo onekana mjengo huo pichani
Mario Balotelli is a magnet for rumours and speculation, so we're not sure what to believe on this one.
According to various accounts on Twitter, the Liverpool striker has found a new home in Helsby, Cheshire.
The property in question—as per Whoateallthepies—has a list price of £4.75 million and comes with a football pitch in the front garden.
Next Post Previous Post
Bukobawadau