Bukobawadau

MZEE ABBAKAR GALIATANO ATIMIZA MIAKA 85

 'Mungu Atosha' ndilo jina la kwanza kabisa alilopewa na Wazazi wake pale tu alipozaliwa  mnano Sep 14,1929 akiwa mtoto wa Kwanza kwa Baba yake, Marehemu Rajanu Galiatano na Mama yake marehemu Halima Binti Mkwabi.

Ni Mzee Alhaji Abubakar Rajabu Galiatano anayetimiza miaka 85 ya kuzaliwa kwake leo Sep 14,2014 na sasa tupo Nyumbani Kwake Kijijini Buganguzi -Muleba kushiriki  Dua Maalum iliyo andaliwa na familia yake kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema kwa kumwezesha kutimiza miaka 85.
 Yupo Sheikh Mustafa Sadik, pia Mufti wa madhehebu ya Imam Shafih.
 Mzee Galiatano anasema;'leo hii mimi nimetimiza umri wa miaka 85 tangu tarehe niliyozaliwa, hii ni neema kubwa aliyoniruzuku Allah'.....
 Anaendelea kusema;'Katika umri huu nimeona na kufanya mengi aidha nimefanyiwa mengi na hasa mazuri na watu wengi nilioshiriki nao kufanya shughuli za kuendeleza maisha.
 Anapokea zawadi kutoka kwa Mwanae Mama Totos.
 Mzee anasema;'Ninamshukuru Allah kwa kwa yote hayo,Allah alinijalia kuoa, Allah aliniruzuku watoto 24 na 18 kati yao wako hai na wengineo wako hapa(naomba wasimame na watowe Salaam)
 'Allah alinijalia kupata masikani,Allah alinijalia kupata kipandio,Allah alinijalia fursa ya Maisha kwa kunipa riziki ya kukidhi haja na mahitaji ya msingi na ziada.'..Anasema Mzee Alhaji Abbakar Galiatano

Mh. Massawe anatoa neno kabla ya kumkabidhi zawadi mzee Galiatano.

Mzee Pius Ngeze anatoa machache anayo yajua kutoka kwa rafiki yake .
Sheikh wa Mkoa wa Kagera Sheikh Haruna Kichwabuta akitoa nasaha zake.
Mtoto wa Kike wa Mzee Abbakari Galiatano Mh. Afisa akisoma Wasifu wa Baba yake mpendwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.Fabian Massawe Mgeni Rasmi katika Shughuli hii.
Mzee Pius Ngeze, rafiki  mkubwa 'Katikilo' wa Mzee Abbakari Galiatano.
 Mzee Salum Ally Al-Saqry Organizer  Mawingo ndiye Mc Muongozaji wa Shughuli hii.
Mzee Maulid Kambuga. 
Ndugu Hassani Khraish na Ndugu Hamza Ngemera.
Mr. Twaha Msoke, Mzee Kakobe wa Nshamba na Ndugu Lwakatale MULEBA
Kulia ni Mdau Abdul Galiatano.
 Mtu na Mdogo wake pichani, ni Ma Zuliath  Rajab Galiatano na Kaka yake katika nyuso za furaha.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.Fabian Massawe ameshiriki katika ya Mzee wetu Haji Abbakari Galiatano,iliyo andaliwa kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema kwa kumwezesha kutimiza miaka 85. 
 Mh. Massawe ametoa pongezi hizo kwa Haji Abbakari Galiatano na kumkabidhi zawadi na kusema kwamba ;'anatambua umuhimu wake katika historia kwa ushirikiano wake naViongozi wetu katika kudai uhuru wa Tanganyika '
Mh. Nazir Kalamage na mkuu wa mkoa mstaafu Mzee Ahmed Kiwanuka
Mama Sadath  katika pozi pichani
Mh. Massawe, Eng Laurian Rwebembera na Mzee Pius Ngeze
Komredi Majid Kichwabuta.
 Sheikh Fakhrudin Mustapha ambaye ndiye Mkuu  wa Shule Sekondari ya Seminari ya Kiislamu Katoro.
Binti Warda Nuru Galiatano.
Bi Aida Ababakari Galiatano. Mwl. Adia Galiatano, Mama Sadath na Dkt Anath  katika picha na wageni wengine ukumbini
Kamuda A.Galiatano na Mh. Afisa A. Galiatano.
Mama Tahimri pichani kulia.
 Mmoja wa waalikwa wa Kijijini Buganguzi.
 Mdau Ramadhani Kambuga, akifuatilia kwa umakini kinacho endelea.
Sheikh Haruna Kichwabuta na Alhaji Galiatano pichani.
 Mama Aisha 'Bi Sauda' na Mama Mwahija.
 Nani Kama Baba nani kama babaBi Jeanifer Murungi Kichwabuta akiongozana na ndugu wanafamilia kwa Vikereshendo ,hoi hoi
 Wakati mengine yakiendelea...
 Kikubwa mzee Galiatano ametumia fursa hii kuwahusia watoto wake , jamaa zake na watu wote walio hudhulia kuwa  pendaneni,shirikianeni,Saidianeni, amrishaneni kutenda mema na kukatazana mabaya,epukaneni ubaguzi wa namna yoyote, Sisi Sote ni Wamoja.
 Shangwe za hapa na pale ukumbini
 Mama Muhazi akikabidhi zawadi yake kwa Mzee Galiatano
Mr Bashir akimpongeza Mzee Galiatano mara baada ya kumkabidhi zawadi
Mama Nurath, Mrs Nurag akiongezana na Mama Zahituni, hii ni sehemu ya 'Wakamwana'

Madarasa ikiendelea kutumbuiza.
Ndugu Jumanne Bingwa pichani katikati.
Mzee Isaaka Selemani Galiatano akiserebuka na Qaswida.


Mh. Eng. Rwebembera akitetta jambo na Mzee Ngeze.
 Bi Aida Ababakari Galiatano. Mwl. Adia Galiatano, Mama Sadath na Dkt Anath  katika picha na wageni wengine ukumbini
Bi Safura Issak Seleman Gakiatano, pichani katikati.
Taswira mbalimbali wakati Shughuli ikiendelea.
Kushoto ni Mama Muhazi, akifuatiwa na Mh. Mwajabu na Mh. J. Mrungi
Ndugu Jumanne Bingwa rafiki wa familia ya Mzee Abbakar Rajabu Galiatano
Matukio ya zawadi kutoka kwa Watoto , Wajukuu na Vijukuu  yanafuata hivi punde.
Mrs Hamis Selemani Galiatano, huyu ni BI Harusi ambaye shughuli yake imefanyika sambamba na shughuli ya miaka 85 ya Mzee Galiatano
 Sheikh Mustapha Sadik  akitoa neno kwa lugha ya Kiarabu


Sheikh Idrisa katika kisomo
Moja ya Zawadi aliyo kabidhiwa na mwanae Dkt Anath
 Hivi ndivyo mambo yalivyojili ndani ya Viwanja vya Masjid Nusurath,Kijijini Buganguzi


 Mama Ibra , Bi Najiath na Mama yake Mdogo pichani Bi Afisa.
Mh. Mwajabu na Wifi yake Bi Sofia.
 Mambo yanaendelea kuwa mambo.Endelea kuwa nasi


 Dkt Anath katika picha na Baba yake Mzazi.
KIPENGERE CHA PICHA 10 KATIKA MENGINEYO IKIFUATIWA NA SEHEMU YA VIDEO.
 Khadja Abbakari Galiatano katika mengineyo.
 Kijana Sadath Galiatano katika Ukodak na Mkali Salum Galiatano (CEO) of Nyumbani Studio
Ndugu Kabaka , Mdau Majid Kichwabuta na Mh. Mzee Nazir karamage.
 Eng. Rwebembera akitoa neno kwa niaba ya wakwe wa Mzee Galiatano
SEHEMU YA KWANZA VIDEO NENO LA MZEE GALIATANO
SEHEMU YA PILI VIDEO ZAWADI YA MKUU WA MKOA.F.MASSAWE. MATUKIO YA PICHA YANAENDELEA SOOOON..
Next Post Previous Post
Bukobawadau