Bukobawadau

NI MARA CHACHE SANA KIPATO CHA MTU KUZIDI UELEWA WA MTU HUYO

Wakati mmoja tajiri alisema: kama fedha zote duniani zikikusanywa na kugawiwa sawa kwa watu wote, baada ya kipindi kifupi, fedha hizi zitakuwa zimerudi mifukoni mwa matajiri walionazo leo!!!
Ni vigumu sana, kutunza na kumiliki kwa kwa muda mrefu, mali au utajiri ambao haukutokana na kuongezeka kwa uelewa wa mtu husika.

maisha ya mtu sasa, ni matokeo ya uelewa wa mtu wa jana.....hili mtu huyu awe na maisha tofauti kesho, basi ni sharti mtu huyu aanze kuongeza uelewa LEO.
1. Kwa nini watu wawili wafanyao kazi katika kampuni moja,wanao umri sawa,wametoka mtaa mmoja, wanapata vipato tofauti?... mmoja milioni tano,na mwingine laki mbili?....hawa watu wawili wanao uelewa tofauti!!!!
2. wakati mwingine watu uendelea kujiliwaza, labda watu wanaofanya vizuri wanao muda mwingi wa siku, hata hivyo watu wote tunayo masaa sawa ya siku( masaa 24),.....kumbuka, inapofika saa sita usiku,MUNGU ujaza tena kapu la kila mtu masaa sawa, akitegemea mtu huyu amejifuza vyema siku iliyopita jinsi ya kutumia muda wake!!!!!! pia leo kuna vijana wengi wanao wazidi vipato wazazi wao, waliofanya kazi ileile!..........labda wanaofanikiwa sana wametokea katika familia tajiri, walisoma shule bora, hata hivyo uhalisi unaonesha kuwa watu wengi wanaomiliki utajiri mkubwa wana elimu ya darasani ndogo!!!!
3. utamsikia mtu anasema, kama ningelikuwa na muda wa kutosha maisha yangu yasingelikuwa hivi, kama ningelikuwa naishi maeneo fulani ningelifanikiwa sana, kama ningelimuoa mwanamke muelewa maisha yangu yasingelikuwa hivi, kama nisingelikuwa na familia na watoto,ningelifanikiwa......kama ningeli.......hata hivyo, hizi zote ni lugha za kujilewesha na maneno, na hivyo mtu husika kushindwa kuchukua hatua sahihi, kwa kujiliwaza na maneno yasiyo na mshiko.
SASA KAMA MTU HAWEZI ONGEZA MASAA YA SIKU, HAWEZI BADILISHA NYAKATI, HAWEZI BADILISHA MAZINGIRA, HAWEZI BADILISHA UMBO LAKE....AFANYEJE ILI MAISHA YAKE YABADILIKE?
JAMBO KUBWA NI KUHAKIKISHA KILA SIKU MTU HUYU ANAONGEZA THAMANI YAKE.
kumbuka kila mtu analipwa sokoni kulingana na thamani aliyonayo hapo sokoni....stori hii fupi inatuonesha ukweli huu:
Nick, kijana wa nchi ya Australia, aliyezaliwa hana mikono, hana miguu.....hata hivyo kijana huyu sasa ni tajiri mkubwa sana huko marekani!!!

Kumbe ulemavu wa viuongo, unene, uwembamba, ufupi, urefu, na sura bora....vyote hivi havina nguvu ktk kusababisha mtu kuongezeka kimaisha....ulemavu mkubwa wa mafanikio unaanzia kwenye uelewa.
Badala ya Nick kijana mlemavu wa viungo kuangalia udhaifu alionao, yeye aliamua kuangalia nguvu ya vichache alivyo navyo na kuvitumia vema, na hivyo kuweka historia kubwa.

TATIZO LA WATU WENGI NI KULALAMIKA NA WASIVYO NAVYO, BADALA YA KUANGALIA VILE WALIVYONAVYO NA KUAMUA KUVITUMIA VYEMA....KILA MTU KUNA KITU ALICHONACHO LEO, AMBACHO AKIANZA KUKITUMIA VEMA, MAISHA YA MTU HUYU YANABADILIKA KABISA.....EBU PATA DK CHACHE UJIULIZE, UNA NINI MKONONI?
NA HILI UJUE NGUVU YAKO HALISI, LAZIMA UCHUKUE MUDA WA KUTOSHA KUJIFAHAMU, BADALA YA KUCHUKUA MUDA MWINGI KUWAFAHAMU NA KUWA MASHABIKI WA WATU WENGINE......tuliwashabikia watu wengi tangu hapo awali.....wapiganaji wakubwa, wachezaji wakubwa, wanasiasa wakubwa, matajiri wakubwa, wanamziki wakubwa, waigizaji wakubwa......hata hivyo watu wale wa kale, sasa hawapo tena kwenye ramani, wamejitokeza wengine ambao nao watapita....kamwe mfumo huu hautakwisha..
Cha kujiuliza ni lini utaanza kuwa shabiki wa maisha yako na kipaji chako?

EBU TUPATE MUDA WA KUWA MASHABIKI BORA WA VIPAJI NA NDOTO ZETU, NA HUU NDIO USHABIKI BORA TUTAKAO DUMU NAO MPAKA SIKU TUNAPUMUA PUMZI YA MWISHO.
TUNAWATAKIENI JUMAMOSI NJEMA
Next Post Previous Post
Bukobawadau