Bukobawadau

SAKATA LA MTOTO 'HAPPINESS' ANAYEPAA KIMIUJIZA

Stori: Richard Bukos
MTOTO Happiness (10) (pichani) ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita  alizua kizazaa mjini Zanzibar baada ya kuonekana akizungumza na viumbe wa ajabu na wanyama, ametua jijini Dar kufuatia kufika kisiwani humo kimaajabu.
 Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo, Sarah Zefania, mwanaye Happiness alianza kuonesha maajabu Zenji tangu alipoonekana kwenye uwanja wa ndege kisiwani humo wiki iliyopita.
Alisema maofisa wa uwanja huo walipigwa butwaa baada ya kumwona mtoto huyo uwanjani amepita sehemu zote za ukaguzi ambazo abiria asiyekaguliwa nyaraka zake za kusafiria na mitambo maalum ya kuangalia vitu mbalimbali vikiwemo kemikali hatari, silaha na madawa ya kulevya hawezi kupita.

Mtoto Happiness akiwa na mama yake mzazi, Sarah Zefania. 
Kwa mujibu wa mama huyo, aliambiwa na maofisa wa uwanja huo kuwa sehemu hizo zote mtoto wake alipita bila kuonekana na kamera za uwanjani hapo wala kuacha kumbukumbu yoyote hali iliyozidi kuwaumiza vichwa maofisa wa uwanja huo.
Zefania alisema wakati maofisa hao wakitafakari hayo, ndipo msamaria mwema mmoja alijitokeza na kumchukua kwenda kumuhifadhi nyumbani kwake.
“Akiwa nyumbani kwa msamaria mwema huyo, nimeambiwa mwanangu alianza kumfanyia maajabu mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wanyama na viumbe wengine wa ajabu au kutoka nje huku mlango umefungwa kwa ndani.
“Kuna muda alizungumza na viumbe wasioonekana ambapo aliwasiliana nao na kumletea vitu kadhaa alivyovitaka. Wakati mwingine alizungumza na wanyama wa mle ndani, kama kuku na paka ambao alikuwa akiwatuma kumfanyia yote aliyokuwa akiwaagiza.
“Hali hiyo ilimshtua yule msamaria mwema naye aliomba kupambazuke ili ampeleke mwanangu ustawi wa jamii. Yaani nahisi pengine angekuwa amemuokota sehemu bila kukabidhiwa mbele ya mashahidi pengine angemtupa usiku huohuo.

 Mama mzazi wa mtoto huyo, Sarah Zefania. 
Mama huyo alisema alimpeleka mtoto wake shuleni lakini kila akifika harudi nyumbani na kutorokea anakokujua na kuonekana baada ya wiki mbili au tatu.
Kufuatia hali hiyo amewaomba wasamaria wema na viongozi wa dini kumwombea mtoto wake ili arudi katika hali ya kawaida kwani anajua kuna mkono wa mtu wa karibu uliyemharibu mtoto wake.
Next Post Previous Post
Bukobawadau