Bukobawadau

VSO NA PCF WATOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 80 KUBORESHA MAZINGIRA YA UFUNDISHAJI NA KUJIFUNZIA ILI KUINUA KIWANGO CHA ELIMU KAGERA

Mkuuwa Mkoa wa Kagera ameyapongeza mashirika binafsi ya  Vulutary Service Overses (VSO), na Pestallozi Chirdren Faundation (PCF) kwa kunuia kuinua kiwango cha ubora wa elimu katika Halmashaauri ya Wilaya ya Bukoba kwa kutoa  zaidi ya shilingi 80 milioni kuboresha mazingira ya ufundishaji na kujifunzia.
Pongezi hizo zilitolewa na Kanali Mstaafu Fabian Massawe tarehe 21/10/2014 wakati wa hafla fupi ya kutembelea, kukagua na kupokea rasmi kazi zilizotekelezwa na mashirika ya VSO na PSF katika shule za Msingi Nyakato na Kalwoshe Kwenye  Halmashauri ya Wilaya ya  Bukoba.

Mashirika ya VSO na PCF kwa kushirikiana walibuni mkakati wa pamoja wa kuboresha mazingira ya ufundishaji na kujifunzia ambao ulianza mwaka 2011 na lengo kubwa likiwa ni kuweka mazingira bora ya mtoto kujifunzia, kuweka mbinu shirikishi katika ufundishaji kati ya mwalimu na wanafunzi aidha kuandaa zana za kufundishia zenye gharama nafuu.
Aidha mwaka 2013  VSO na PCF kwa pamoja waliamua kukarabati Shule za Msingi Nyakato na Kalwoshe zilizokuwa katika hali mbaya kutokana na shule hizo kuwa kongwe na miundombinu yake ilikuwa tayari imeharibika vibaya sana hadi kupelekea walimu na wanafunzi kunyeshewa mvua wakiwa madarasani na ofisini.
 VSO na PCF wameweza kukarabati vyumba vya madarasa  5 na  ofisi 2 na kubadilisha bati, kujenga vyoo 2 vyenye matundu 8, kujenga matenki 2 ya maji kwa ajili ya wanafunzi kusafisha mikono yao mara watokapo chooni, aidha yalitolewa madawati 144 meza 6 na kabati 1 ya mwalimu katika shule ya Msingi Nyakato.
Shule ya Msingi Kalwoshe VSO na PSF waliweza kukarabati madarasa 3, kujenga makta mpya 1 na vifaa vyake vyote, pia walijenga vyoo 2 vyenye matundu 8, pamoja na matenki mawili ya maji kwaajili ya wanafunzi kusafisha mikono, na kutoa  madawati 44 kwa watoto wa awali pamoja na viti vya walimu.
Aidha VSO na PCF imetoa mafunzo ya elimu ya mbinu za ufundishaji kwa njia shirikishi na kuandaa zana za kufundishia za gharama nafuu ambazo zinapatikana kwenye mazingira husika kwa walimu 48 ambao watatumika kama wakufunzi kueneza elimu hiyo katika mkoa mzima.
 Bi Beatrice Nalingingwa ni Mkurugenzi wa shirika la PCF lenye makao makuu yake nchini Switzeland alisema lengo la shirika lake ni kulinda haki ya mtoto, kutoa elimu bora,   ushirikishwaji wa watoto, na ndiyo maana waliamua kushirikiana na VSO kuboresha utoaji wa elimu mkoani Kagera.
Walimu wakuu wa Shule za Msingi Kalwoshe na Nyakato waliwashukuru VSO na PCF kwa kile walichokifanya na kuwaboreshea mangira ya kufundishia na kujifunzia wanafunzi na kuondoa kero za kunyeshewa mvua darasani na ofisini wakati wakitekeleza majukumu yao.
Kanali Massawe akihitimisha hafla fupi hiyo alitoa wito kwa mashirika mengine nchini kama hayo kutoa misaada ya elimu ili kuupandisha mkoa wa Kagera kielimu. Aidha  alitoa wito kwa walimu kutumia maktaba zilizojengwa kujiendeleza kielimu pamoja na kuweka mkazo kwa nidhamu ya wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuzingatia usafi na unadhifu wa wanafunzi wao.
Next Post Previous Post
Bukobawadau