Bukobawadau

GO PINDA,NENDA TU MZEE WANGU,MPE FURSA JK AUNDE BARAZA JIPYA!

Na Nova Kambota, 0712- 544237
Tofauti na wengi wanavyodhani, mzee wangu Pinda ulishaonyesha dalili
za wazi ikiwa kweli unamudu vyema nafasi ya uwaziri mkuu. Kuna mengi
tu yaliyofanya baadhi yetu tutilie shaka umahiri wako lakini hii
skandali ya Tegeta/Escrow imefunga mjadala!

Unakumbuka uliposema na wapigwe tu? Liwalo na liwe!
Wakumbuka ile kauli ya tumechoka?
Wakumbuka mgomo wa madaktari?
Je wakumbuka kauli yenye utata “anayeua albino na yeye auwawe”?
Lakini wajua namna “mchwa” katika baadhi ya halmashauri wanavyotafuna
fedha za wananchi?

Tegeta/Escrowni hitimisho la yote haya, mzee wangu Pinda mtoto wa
kulima, let it go! Jiuzulu, mpe fursa rais Kikwete aunde baraza jipya
la mawaziri, urais unaweza kutafutwa hata nje ya uwaziri mkuu!

Ukiwa mwanasheria utanielewa vizuri naposema hoja si ikiwa unahusika
au la! Hili si muhimu sana, hoja hapa ni dhamana ya uongozi kusimamia
shughuli za serikali ilishindwa kutumika kunusuru “skandali”hii.
Kiongozi waumma “kutuhumiwa” si jambo jema, tuhuma pekee zinatosha
kukufanya ubwage manyanga “resigning does not mean you are weak, but
sometimes it means you are strong enough to let it go”

Achia ofisi ya umma kwa manufaa ya walala hoi wa Tanzania, kiongozi wa
umma umetuhumiwa kutosimama kidete kuzuia uozo huu kabla, kauli za
“kila mtu atabeba msalaba wake” si za kulisaidia taifa, ni kauli
inayoashiria hamu ya mtawala asiyependa kuwajibika, anayetaka
kung’ang’ania madaraka! Haifai kabisa, busara inakutaka kuwajibika
kama mtangulizi wako Edward Ngoyai Lowassa, kumbuka “Caesar’s wife
must be above suspicion’’

novakambota@gmail.com
Next Post Previous Post
Bukobawadau