Bukobawadau

KATIKA PICHA RAIS KIKWETE AKITOKA HOSPITALINI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Daktari Bingwa Edward Schaeffer kutoka Hospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita.Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Daktari Edward Schaeffer muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anaendelea na matitabu yake nchini Marekani, leo, Jumatano, Novemba 12, 2014, anatarajiwa kutoka wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye Hoteli Maalum ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.

Rais Kikwete amekuwa kwenye Hospitali ya Johns Hopkins tokea Jumamosi iliyopita wakati alipofanyikwa upasuaji wa tezi dume (prostate) na afya yake imekuwa inaimarika kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea.

Kutokana na kuondolewa kwa bandeji kwenye mshono ambao nao umeanza kukauka vizuri, Rais Kikwete baadaye leo atahamishwa kutoka wodini kwenda kwenye Hoteli Maalum yenye uhusiano na Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko karibu na hospitali hiyo.

Akiwa kwenye Hoteli Maalum hiyo, Rais Kikwete ataendelea kupatiwa matibabu, kutembelewa mara kwa mara na madaktari na kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi muda wote. Wiki moja baadaye, Rais Kikwete atafanyiwa tathmini ya kuwawezesha madaktari kuamua hatua inayofuata ya matibabu yake.

Wakati huo huo, kwa sababu ya wingi wa ujumbe mfupi wa simu (sms) ambazo amekuwa anazipokea Rais Kikwete, imeanzishwa namba maalum ya simu ambako wananchi wanaweza kuwasiliana kwa sms na Mhe. Rais. Namba hiyo ni +1-646-309-2295.
Next Post Previous Post
Bukobawadau