Bukobawadau

SHEKHE PONDA AACHIWA HURU

Askari wa Magereza akimfungua pingu Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu., ambapo leo yeye na wenzie 49 wameachiwa huru ila watatumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja. PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA
 HATIMAYE katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili.

Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.

Mara baada ya kutolewa hukumu hiyomahakamani hapo pali ibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama hiyo.
Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
1.Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya aridhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo umiliki.
2.Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
4.Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.
5.Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. Awasihi Waisilamu kufuata taratibu za kisheria ili kuipata mali hiyo halali itumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
 Askari wakiwa kwenye msafara wa kumsindikiza Sheikh Ponda baada ya kuachiwa.
 Sheikh Ponda akiswali katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam.
 Wafuasi wa Sheik Ponda wakimshangilia alipokuwa akihutubia ndani ya Msikiti wa Mtambani.
 Katibu wa Jumuia za Taasisi za Kiisalamu Tanznania, Sheikh Ponda Issa Ponda akifanya mahubiri katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam, alipokwenda leo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumwachia huru jana, yeye na wenzake 49 waliokuwa wanakabiliwa na shitaka la uchochezi
Next Post Previous Post
Bukobawadau