Bukobawadau

VETA KUCHELEWESHA VYETI

 Habari za kazi naomba uiwekee kwenye mtandao ili wahusika waweze kuisoma kirahisi.
Lalamiko langu kubwa ni kuhusu VETA kumekuwa na tatizo la ucheleweshaji wa vyeti pindi wahitimu wanapomaliza course zao siju nikwanini? 
Tukiangaliwa vyuo vingi vinavyomilikiwa na serikali wanafunzi wanapomaliza shule yao na matokeo yao yakatoka uwa wanapewa result slip inayoonyesha kuwa huyu mtu amemaliza course fulani na ameshinda wakati anasubili cheti chake na cheti hakichelewi sana kutoka kama ilivyo kwa VETA kitu ambacho ni tofauti na VETA mwanafunzi anapomaliza course yake na matokeo yakatoka amefauru anasubili cheti karibu mwaka mzima sasa huyo mwanafunzi au mhitimu kama anatafuta kazi ataipataje bila cheti? au atafanyaje maombi katika vyuo vingine kwa ajili ya kujiendeleza? Jamani tunaomba milifanyie kazi maana sio kawaida kabisa ni uonevu hasa kwa vyuo vya mikoani kazi zenyewe zimekuwa ngumu bila cheti cha uhakika sio rahisi kupata kazi.
TUNAOMBA WAHUSIKA WALIFANYIE KAZI
Nimewasilisha
Next Post Previous Post
Bukobawadau