Bukobawadau

DK MASSABURI AFUNGUKA SAKATA LA ESCROW KWA MARA YA KWANZA


 SEHEMU YA VIDEO HAPO JUU DK MASSABURI AKIONGELEA  SAKATA LA ESCROW
 Dk. Massaburi:

Tusimtwishe Rais Kikwete mizigo mizito
WATANZANIA wameombwa kumuonea huruma na kumpongeza Rais Jakaya Kikwete, kutokana na kufanya kazi kubwa ya kuiletea Tanzania maendeleo katika kipindi cha miaka 9 ya uongozi wake, na si kumkatisha tamaa kwa kumtwisha mizigo mizito.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ALAT), Dk Didas Massaburi aliyasema hayo wakati alipokuwa anazungumzia mzigo mkubwa aliokabidhiwa Rais Kikwete wa kutekeleza maazimio manane ya Bunge kuhusu sakata la madai ya kuchotwa kwa fedha zinazodaiwa kuwa ni za umma katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
 

Dk Massaburi alisema hivi sasa suala la Escrow limeleta mtafaruku na madhara makubwa ndani ya nchi kutokana na kupotoshwa na kikundi cha watu wachache wenye maslahi binafsi, hatua ambayo sasa inamfanya Rais kuacha kushughulikia maendeleo ya nchi na kulishughulikia suala hilo.
“Tufike mahala tuache kumbebesha Rais wetu mizigo mizito na isiyo na sababu kwani amefanya mambo mengi na makubwa na yanayogharimu matrilioni ya shilingi katika ujenzi wa barababara, umeme, maji na elimu.

“Leo hii kutokana na sakata la Escrow ambalo fedha zinazodaiwa kuwa ni za serikali haziwezi hata kujenga barabara mbili za lami, nchi inapita katika wakati mgumu sana,” alisema Dk Massaburi.
Alisema ALAT kama mdau mkubwa wa maendeleo katika serikali za mitaa na hasa vijijini inaguswa na sakata hilo kwa vile sasa serikali inaendelea na kazi kubwa ya kupeleka umeme vijijini na hakuna maendeleo yanayoweza kufikiwa vijijini bila nishati ya umeme.
Alisema suala la Akaunti ya Tegeta Escrow limepotoshwa na watu wenye maslahi binafsi yakiwemo ya kutaka kukubalika kwenye nafasi za Ubunge, Umeya na hata Urais na kwa bahati mbaya wananchi wameingiwa na imani kali kuhusu upotoshaji huo na kujenga chuki kubwa kwa serikali yao.

 “Hali imekuwa mbaya sana bila sababu ya msingi, watu wanashindwa kufanya shughuli muhimu za maendeleo kwa suala la Escrow. Imefika mahala tunaweka shinikizo la kutaka kuwajibishwa kwa viongozi wachapa kazi na walioliletea maendeleo makubwa Taifa letu kwa masuala yanayopotoshwa tu, jambo ambalo ni la hatari sana kwa mustakabali wa Taifa letu,” alisema Dk Massaburi. 
Alisema mbali ya wanasiasa, taasisi za kifedha za kigeni pia zinalishabikia suala hilo kutokana na ulafi wa kutaka kuzichukua fedha hizo na wala si kuwapa wananchi na pia kampuni za kigeni za umeme ambazo zinaathirika na bei ndogo ya umeme inayouzwa na IPTL ukilinganisha na wao, zinahusika.
“Kwa bahati nzuri mimi nimeisoma vizuri sana taarifa ya CAG, hakuna mahala anaposema fedha ni za umma. Fedha ya umma inajitokeza katika ulipaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na ambayo kwa kawaida kodi hii hulipwa na aliyelipwa.
“Mimi nikilipwa fedha leo, napokea kwanza hundi yangu halafu baada ya kuchukua fedha na kuwa mikononi mwangu ndio mwisho wa mwezi nakwenda kulipa kodi ya VAT, hawakati fedha hiyo moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yangu. TRA wanapaswa kuifuatilia kodi yao maana hapa ni suala la sheria ya Kodi kukiukwa hakuna Sheria ya Escrow,” alisema Dk Massaburi. 

Alisema kwa namna taarifa ya CAG ilivyofafanua hakuna ubishi kwamba IPTL sasa inamilikiwa kihalali na Kampuni ya PAP, na hivyo ni lazima kama Taifa kuipa ushirikiano kampuni hiyo kuendelea kuzalisha umeme na kuuza kwa bei nafuu na si kushinikiza kutaifishwa kwa mitambo hatua ambayo italiingiza Taifa kwenye matatizo makubwa ikiwemo kurejea kwenye bei kubwa ya umeme.
“Mazungumzo kuhusu Escrow ni ya miaka mingi sana, yalianza tangu enzi za Ngeleja (William- aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini. Watu hawa wamezungumza suala hili kwa zaidi ya miaka minane.Leo hii mtu anapotosha kwamba makubaliano ya kuondoa fedha kwenye akaunti ya Escrow yalifanywa siku moja tu pale Kunduchi Beach.
“Tuwasaidie viongozi wetu wanaofanya kazi nzuri ili kulikoa Taifa letu. Rais anafanya kazi nzuri, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda ) anafanya kazi nzuri, Waziri Muhongo anafanya kazi kubwa na nzuri. Hawa ni watu muhimu sana kwetu,” alisema Dk Massaburi ambaye alitangaza kutokuwa na mgongano wa kimaslahi kwa sakata hilo. 

NANI WA KULAUMIWA
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kutokana na uzoefu wake katika masuala ya hisa za kampuni, amegundua kuwa sakata ta escrow linachochewa na makundi mawili.
“Kundi la kwanza ni wapotoshaji wakiwamo wabunge, wachumi ambao walikuwa wakisambaza upotoshaji huo kwa masilahi yao binafsi...mtu mwingine anaweza kusema ninatetea labda nimepata mgao, hapana...ila ukweli unatakiwa uelezwe wazi.”
Dk Massaburi alitaja kundi lingine aliloliita la fisi ambalo lina idadi kubwa ya wapambe waliokuwa na njaa ya kupata mgao huo.
Alisema hakuna kiongozi anayetakiwa kuwajibishwa kutokana na ukweli kwamba, Kampuni ya Mechmar ndiyo iliyosababisha kuwapo kwa tatizo hilo.
Mwaka 2010, kampuni ilikabidhi umiliki wake wa asilimia 70 ya hisa za IPTL kwenda kwa Kampuni ya Piper Link
Next Post Previous Post
Bukobawadau