Hata kama kwenu mnajiweza
kiuchumi na kifursa kuliko walivyo kwa mume wako au kuliko alivyo yeye,
hata kama ulibahatika kwenda darasani kuliko yeye, bado wewe ni mke na
haunabudi kumheshimu mume wako kama mume. Nafasi ya juu kijamii, upana
wa elimu, uwezo wakifedha au kifursa havitoshi kamwe kufanya utake
kuogopwa na mumeo au na wanaokuzunguka, havikufanyi wewe ndio uwe mtoa
“orders” na kutaka kila kitu kifanyike unavyotaka wewe.
Nadhani labda
bado hujajua maana halisi ya kuwa “mke”, kama kweli ulimpenda na
unamheshimu kama mume na kiongozi wa familia yenu basi vitu na hali
zozote za kwako au kwenu hazitaishinda nguvu ya penzi na kwahivyo
hautopata shida kumheshimu na kumjali kama MUME, lakini kama kuolewa
naye kulilazimishwa na mazingira (kama vile mimba, kujiona unachelewa
kuolewa, kushawishiwa n.k) basi lazima dharau itautangulia utu wako.
Hata kama wazazi wako wanamdharau, na kumpinga mumeo kwasababu walitaka
uolewe na mtu wakufanana na hadhi ya familia yenu, bado wewe haunabudi
kusimama upande wa mume wako na kuwaonyesha wazazi wako kuwa haukukosea
kumfanya yeye chaguo lako. Sasa inakuwaje unasimama upande wa wazazi
wako na kumshushia hadhi mumeo? Huyo sio tu baba wa watoto wako, huyo ni
mumeo, usijitafutie balaa usizozijua na kuifunga milango mingine ya
Baraka na mafanikio kwa tabia hiyo mbaya. Love surpasses everything
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Yap,nimekupata mtu wangu but ndoa bora ni nyote wawili kueshimiana na kusaidiana kwa kila jambo
Post a Comment