MTOTO AOKOLEWA NDANI YA SHIMO LA CHOO
Mtoto
wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja ameokolewa na
wasamaria wema toka kwenye shimo la choo akiwa bado hai bada ya mama
yake mzazi kumeza dawa kwa lengo la kutoa mimba na kumtupa ndani ya
shimo hilo.
ITV imefika katika kituo ch afya cha PK kilichopo kibaoni tegeta
manisipaa ya kinondoni jiji la Dar-es-salaam na kukutana na harakati za
wahudumu wa afya wakijaribu kunasua mabaki ya kinyesi kwenye mwili wa
kiumbe huo,aliyetupwa kwenye shimo la choo katika eneo la tegeta
machakani.
Wakiongea na ITV baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mama
aliyekuw ana muhifadhi kwa muda binti anayedaiwa kutupa kichanga hicho
wamesema kuwa watoto walipata taarifa ya mlio wa sauti wa mtoto
ukisikika toka kwenye choo cha shimo kabla ya kuchukua hatua za kuvunja
choo hicho na kutoa mwili wa kiumbe huyo.
Bi Aisha Mohamedi anayedaiwa kutupa kichanga hicho kwenye shimo la
choo amesema kuwa,awali mzazi mwenzake alimlazimisha kutoa mimba hiyo
bila mafanikio na hata kudiriki kumtishia kwa silaha aina ya kisu,na
ndipo alipozidiwa na kupewa vidonge na mzazi mwenzake kwa minajili ya
kutoa ujauzito huo na kukiri kujutia kosa lake hilo.
Mganga mfawidhi katika kituo cha afya cha PK Dkt Mashaka Mwanula
amethibitisha kupokea mtoto huyo wa kiume aliyeokolewa baada ya kutupwa
ndani ya choo na hivyo kumpatia huduma ya kwanza kwa kumsafisha huku
wakitarajia kumpeleka katika hosip[itali ya wilya ya kinondoni
mwananyamala kwa uchunguzi zaidi wa afya ya mtoto huyo,juhudi za kumpata
kamnada wa polisi mkoa wa kipolisi kinondoni ACP Camilius Wambura
kuthibitisha tukio hilo zinaendelea.