Bukobawadau

LIPUMBA:Walioshindwa kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa wawajibishwe.

Chama cha wananchi -CUF- kimemtaka rais Jakaya Kikwete kumuwajibisha waziri mkuu na waziri wa tamisemi kwa kushindwa kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa na baada ya kuibuka dosari kubwa zikiwemo kukosekana kwa wino, majina ya wananchi na karatasi za kupigia kura jambo lililote vurugu na kusababisha vituo vingi kurudiwa uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa CUF taifa Prof. Ibrahim Lipumba ametaka serikali kutekeleza makubaliano ya vyama vya siasa na tamisemi yaliyotaka uchaguzi tume ya taifa ya uchaguzi ndio iwe na dhamana ya kusimamia uchaguzi, pamoja na daftari la wapiga kura litumike katika uchaguzi wa serikali za mita pamoja na kuingizwa kwa kipengeke cha maadili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
 
Aidha kutokana na vurugu zilizojitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika baadhi ya maeneo, Profesa Lipumba amelitahadharisha jeshi la polisi kuhacha kutumia nguvu kwa ajili ya kulinda maslahi ya baadhi ya vyama ili kuepusha vurugu zisizoza lazima katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani.
Next Post Previous Post
Bukobawadau