Bukobawadau

MKUU MPYA WA MKOA WA KAGERA AJITAMBULISHA WILAYANI NA KUKAGUA UJENZI WA MAABARA PAMOJA MIRADI YA MAENDELEO

Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella atembelea Halamashauri za Wilaya za Mkoa wa Kagera kujitambulisha kwa  Madiwani, Watendaji wa halmashauri  za Wilaya pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwa ni pamojana kukagua ujenzi wa maabara katika shule zote za serikali.
Ziara hiyo ilianza Desemba 4, 2014 katika Wilaya ya Missenyi  na kufuatiwa Wilaya za Muleba Kyerwa, Karagwe, Ngara na Biharamulo. Mkuu wa Mkoa John Mongella alitumia nafasi hiyo kuijimbulisha pia kutoa ufafanunuzi wa majukumu makuu na muhimu ya mkuu wa mkoa katika nafasi yake.

Majukumu hayo ni pamoja na kusimamia shughuli zote za maendeleo katika mkoa, kusimamia ulinzi na usalama katika mkoa na jukumu la tatu ni kusimamia utii wa sheria katika mkoa. Katika mikutano aliyoifanya na wadau na watendaji wa Halmashauri aliyatolea ufafanuzi kwa ufasaha majukumu yake.
Katika kutekeleza majuku yake mkuu huyo wa mkoa alifafanua zaidi  juu ya uwajibikaji wa watendaji wa serikali kwa kutumia mfumo uliopo kutoa  huduma za jamii na kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri za Wilaya kwa kila mtendaji kuwajibika katika nafasi yake ya kazi  aliopo.
 John Mongella  alitoa onyo kali kwa watendaji wa Halmashauri ambao hawatimizi wajibu wao wa kwenda  vijijini kufuatilia maendeleo ya wananchi, alisema atakikisha anawachukulia hatua kali pale itakapobainika kuwa kazi yao ni kushinda ofisini bila kwenda kwa wananchi.
Aidha alitoa maelekezo kwa watendaji wa kata na madiwani  kuwa na siku maalum za kwenda katika halmashauri zao na siyo kila siku kushinda katika ofisi za Wakurugenzi na kufanya kazi za wataalamu. Pia aliwaagiza Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri nao kutenga siku za kukukaa ofisini na siku za kwenda vijijini kufuatilia miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya ofisi zao.
Ujenzi wa Maabara: Mkuu wa Mkoa John Mongella pia alitembelea na kukagua ujenzi wa maabara tatu kila shule ya serikali unavyotekelezwa mkoani Kagera ambapo mwisho wa kukabidhi maabara hizo ulikuwa Desemba 9, 2014 kulingana na agizo la Rais Jakaya Kikwete la mwaka jana Februari 2013.
Katika Halmashauri za Wilaya za Missenyi, Muleba, Kyerwa, Karagwe, Ngara na Biharamulo ujenzi wa maabara katika shule zote za serikali unaendelea ambapo vyumba  vitatu vya masomo ya Fizikia, Kemia na Biologia vinaendelea kukamilishwa ikiwa ni pamoja na miundombinu ya maji na gesi ndani yake.
 Mkuu wa mkoa John Mongella pamoja na kukuagua na kupima na kuhakikisha maabara hizo zinajengwa kwa kufuata michoro ya serikali pia alikuwa akijihakikishia kama vipimo vinafuatwa na kila kitu kinachooneshwa kwenye ramani za majengo hayo kimewekwa kama ramani inavyoonesha,  aidha aliagiza ifikapo January 2015 kila maabara iwe imekamilika tayari kwa  wanafunzi kuzitumia maabara hizo.
Miradi ya Maji: Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella hakusita kukagua miradi ya maendeleo ambayo imeshindwa kukamilika kwa mwakati hususani miradi ya maji katika Halmashauri ya Wilaya  ya Muleba  ya vijiji 10 na miradi ya Quick win katika vijiji vinne vya Kamachumu, Izigo, Rwanda na Itoju.
Katika miradi hiyo ambayo tayari serikali imetoa mamilioni ya fedha imeshindwa kukamilika kwa  wakati na kupelekea wananchi katika maeneo hayo kuendelea kupata adha ya maji jambao ambalo lilimfanya Mkuu huyo Mkoa kuwaagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi na kumpelekea taarifa baadaya wiki mbili.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mkuu wa Mkoa John Mongella alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuhakikisha mradi wa maji wa Ngara mjini unakamilika na kufanya kazi ifikapo  Januari 30, 2015 mara baada ya kugundua kuwa tayari milioni 30 zilitumika ndivyo sivyo.
Aidha alimwagiza mweka hazina wa halmashauri hiyo kuhakikisha mapato ya ndani ya mwezi Desemba 2014 yanaelekezwa katika mradi huo ili huduma ya maji ipatikane haraka katika mji wa Ngara. Pia Mkurugenzi wa halmashauri ya Ngara kuhakikisha anasimamia kesi ya ubadhilifu wa milioni 30 ili mhusika awajibishwe kisheria.
Next Post Previous Post
Bukobawadau