Bukobawadau

CHUKUA SOMO WALA USIJIBWETEKE!

Hatakama amekuahidi kila ulichowahi kutamani, hatakama amejitambulisha kwa ndugu zako wote, hata kama wazazi wako wamemkubali, hata kama ana vigezo vyote vya mume uliyewahi kumdhania au kumuota, hatakama amekwisha kuvisha pete ya uchumba na hata kama mmeanza maandalizi ya ndoa, fahamu kwamba kama tabia zako bado haziendani na tabia za mke ingawa wewe ni mwanamke bado anaweza akaahirisha mpango wakuoana na wewe bila kujali mmefikia wapi. Usisahau kwamba sio kila mwanamke anatabia za mke, ingawa kila mke ni mwanamke. Wanaume wanafahamu pakuoa, na nani anastahili kuwa mke, na nani hastahili, ingawa wanaweza kukudanganya kwa kila neno tamu ila ukweli wanao wenyewe moyoni kwamba huyu ni wakupumzikia tu, na yule ni wakuoa, kwani haujawahi kwenda kwenye harusi ya kijana mliyedhani atamuoa flani lakini siku hiyo mnona kamuoa mtu mwingine na wala hamumfahamu anakotokea wala walikokutana? Au umesahau kwamba kila mchezaji ana nguo za mazoezi na za mechi? Sasa jiulize wewe ni wamazoezi au wewe ni wa mechi, akili mukichwa, badili tabia, ishi na kuwa kama mke sio tu mwanamke, lasivyo utaishia kuwa “maid”, au “matron” au msindikizaji na mhudhuriaji wa harusi za wenzako – Chris Mauki
Next Post Previous Post
Bukobawadau