Bukobawadau

WAFUASI WA CUF 30 WAFIKISHWA KORTINI

Wafuasi 30 wa CUF wafikishwa kortini kwa tuhuma za mashtaka matatu likiwemo la kufanya mkusanyiko usio halali.
Wafuasi 30 wa chama cha wananchi (CUF) akiwemo naibu mkurugenzi wa oganaizesheni, uchaguzi na bunge Shaweji Mketo na mkurugenzi wa mawasiliano Abdul Kambaya wamefikishwa kortini kwa tuhuma za mashtaka matatu likiwemo la kufanya mkusanyiko usio halali, ambapo wameshindwa kutimiza masharti na dhamana na kupelekwa rumande.
Wakili wa serikali Joseph Maugo amedai mbele ya hakimu Emilius Mchauro wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu, jijini Dar es Salaam kuwa washtakiwa wanatuhuma kwa mashtaka matatu ambapo shitaka la kwanza linawakabili washtakiwa wote ambao wanatuhumiwa kula njama ya kufanya uhalifu. Shtaka la pili linawakabili washtakiwa 28 ambao wanatuhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali.
Imedaiwa kuwa walifanya mkusanyiko huo januari 27 mwaka huu, wakiwa katika ofisi ya CUF iliyopo karibu na hospitali ya Temeke bila uhalali wowote walifanya mkusanyiko wa nia ya kufanya maandamano kuelekea viwanja vya Zakhiem, Mbagala, Dar es Salaam.
Katika shtaka la tatu pia linawakabili washtakiwa 28, wanadaiwa kufanya mgomo baada ya katazo halali ambapo washtakiwa bila kujali tangazo lililotolewa na jeshi la polisi la kutokufanya maandamano wao walikaidi wote wamekana kuhusika na tukio hilo huku wakili Maugo akidai upelelezi bado na pia kisheria mashtaka yao yana dhamana.
Mchauro amesema ili washtakiwa wawe nje kwa dhamana wanatakiwa wasaini dhamana ya sh. 100,000 na mdhamini mmoja wa kuaminika, lakini washtakiwa walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande.
Next Post Previous Post
Bukobawadau