Bukobawadau

JK ASIKITISHWA NA MATAMKO YA VIONGOZI WA DINI YA KUWATAKA WAUMINI KUPIGA KURA YA HAPANA KATIBA PENDEKEZWA

Rais Jakaya Kikwete amesema amesikitishwa na kushangazwa kwa kitendo cha baadhi ya  viongozi wa dini kutoa matamko kwa waumini wao ya kuwataka kupiga kura ya hapana kwa  katiba inayopendekezwa  na kuongeza  kuwa hakuwahi kudhani wala kufikiri kuwa kwa  viongozi aliowaheshimu  kama wangeweza Kufanya jambo  kama hilo kwa waumini wao.
Mh.Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini kupitia kamati ya amani ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kitendo walichofanya viongozi hao wa dini  kingeweza kuwa na tija kama katiba inayopendekezwa ingekuwa inawanyima uhuru wa kuabudu.
Na kuhusu mahakama ya kadhi Mh.Kikwete amesema serikali haitaanzisha ila waislamu   wenyewe wana uhuru wa kuwa nayo amala.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es  salaam Mh.Said  Meck Sadick amesema uwepo wa hali ya utulivu hasa katika mkoa wa Dar es Saam  imewezekana  kutokana  na viongozi wa Dini  kuwa naumoja  ambao  kila mara wamekuwa mstari wa mbele  kusaidia  amani idumu nchini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es  Salaam  Alihadi  Mussa Salum amesema mkutano huo unalengo la kujadili  mambo makubwa  yanayolihusu taifa ambapo  makamu Mwenyekiti  wa kamati  hiyo  askofu  Valentino  Mokiwa  amesema  bado  ipo changamoto  ya matumizi ya  Demokrasia iliyopo nchini.
Next Post Previous Post
Bukobawadau