Bukobawadau

ZITTO KABWE BUNGENI LEO

Siku moja baada ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda kusema kuwa Zitto Kabwe ni mbunge halali wa jimbo la Kigoma Kaskazini kutokana na ofisi yake kutokuwa na taarifa rasmi ya kutenguliwa ubunge wake, mbunge huyo leo amehudhuria mkutano wa bunge unaoendelea mkoani Dodoma.
Katika siku hiyo ya kwanza ya kuhudhuria bungeni hapo mara baada ya chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA ambacho alikuwa mbunge kupitia chama hicho kumfukuza uanachama Mhe.Zitto Kabwe amelalamikia hatua ya Serikali kutowatendea haki wakazi wa Kilwa kwa kutowanufaisha na gesi inayopatikana eneo hilo.
 
Katika kikao hicho Zitto Kabwe amesema kumekuwa na malimbikizo ya fedha ambazo kampuni inayohusika na kuchimba gesi katika eneo la Songosongo Wilayani Kilwa ilitakiwa kulipa kwa halmashauri ya wilaya ya Kilwa lakini tangu kuanza kwa uchimbaji huo kampuini husika haijalipa fedha hizo.
 
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa nishati na madini Charles Kitwanga ameliambia bunge kuwa tayari Serikaliimegundua madhaifu hayo na kwamba kwa sasa ipo katika mchakato wa kutathmini halmashauri hiyo inadai shilingi ngapi na hatimaye iweze kulipwa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau